Diwani wa Kata ya Itinje wilayani 
Meatu Mhe.Seni Sitta  Mizumali ambaye ni miongoni mwa waliojeruhiwa 
katika ajali , kwenye Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James 
wilayani Meatu akisaidiwa kuingia kwenye ndege kabla ya kusafirishwa 
kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi 
zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. 
Anthony Mtaka na viongozi wengine wakimsaidia Diwani wa Kata ya 
Mwamanongu wilayani Meatu Mhe.Emmanuel Sayi Mboje ambaye ni miongoni mwa
 waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, 
Kheri James wilayani Meatu kuingia kwenye ndege kabla ya kusafirishwa 
kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi 
zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. 
Anthony Mtaka akizungumzana baadhi ya madiwani waliojeruhiwa kwenye 
ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu
 kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya 
matibabu na uchunguzi zaidi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. 
Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na madiwani sita 
waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri
 James wilayani Meatu kabla ya kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa 
Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi, madiwani watatu 
hawapo pichani kutokana hali za kutoruhusu kusimama walikuwa 
wameshaingizwa kwenye ndege.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. 
Anthony Mtaka(kulia) akizungumza na Diwani wa Viti Maalum Consolatha 
Lushu  katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya diwani huyo na wenzake 
kusafirishwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu 
na uchunguzi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. 
Anthony Mtaka akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo katika 
Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kusafirishwa kwa madiwani  wa Wilaya 
ya Meatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM 
Taifa, Kheri James kabla ya kuwasafirisha kwenda Hospitali ya Taifa 
Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Simiyu,
 Bw.Donald Magesa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo katika 
Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kusafirishwa kwa madiwani  wa Wilaya 
ya Meatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM 
Taifa, Kheri James kabla ya kuwasafirisha kwenda Hospitali ya Taifa 
Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
Viongozi wa Mkoa wa Simiyu 
wakifanya maombi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanzakabla ya kusafirishwa 
kwa madiwani  wa Wilaya ya Meatu waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara 
wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James, kwenda Hospitali ya Taifa 
Muhimbili kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya 
Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akizungumza na baadh ya madiwani 
waliojeruhiwa kwenye ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri
 James kabla ya kuwasafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa 
ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, 
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya madiwani waliojeruhiwa kwenye
 ajali ya Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James kabla ya 
kuwasafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu 
na uchunguzi zaidi.
Viongozi  wa Mkoa wa Simiyu wakiwa
 katika picha ya pamoja katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza baada ya 
kuwasindikiza madiwani tisa waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea kwenye
 Msafara wa Mweyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kwa 
ajili ya kusafirishwa  kwa ndege kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
 ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
Viongozi  wa  Mkoa wa Simiyu 
wakiondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza baada ya kuwasindikiza madiwani 
tisa waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea kwenye Msafara wa Mweyekiti 
wa UVCCM Taifa, Kheri James wilayani Meatu kwa ajili ya kusafirishwa 
 kwa ndege kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na 
uchunguzi zaidi.
………………
Na Stella Kalinga, Simiyu
Madiwani tisa kati ya 11 wa 
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu waliojeruhiwa katika ajali iliyotokea 
Juni 10, 2018 kwenye msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri 
James katika Kijiji cha Kisesa wilayani humo wametolewa katika Hospitali
 ya Rufaa Bugando baada ya kupatiwa matibabu ya awali na kusafirishwa 
kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu na uchunguzi zaidi.
Madiwani hawa walisafirishwa  jana
 jioni wakisindikizwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, 
ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka, viongozi wa CCM Mkoa 
wa Simiyu na viongozi wengine wa wilaya ya Meatu na Bariadi katika 
Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
Wakizungumza kabla ya kuondoka 
Uwanja wa ndege wa Mwanza wametoa shukrani kwa madaktari  na wauguzi 
waliowahudumia toka siku kwanza katika kituo cha Afya cha Mwandoya, 
Hospitali ya Wilaya ya Meatu, Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu na 
Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa namna walivyowahudumia hali 
iliyochangia kuimarisha afya zao.
“Ninashukuru kwa matibabu ya awali
 niliyopewa Meatu na Bariadi  yamenisadia sana, baada yaajali nilikuwa 
na maumivu makali sana lakini kutokana na huduma niliyoipata nina nafuu,
 yamebaki maumivu  ya kifua kwa ndani” alisema Mhe. Pius Machungwa 
Diwani wa Kata ya Ngh’oboko ambaye pia  Mwenyekiti wa Halmashauri ya 
Wilaya ya Meatu.
“Katika ajali ile nilijeruhiwa 
sana maeneo ya mbavu, kiuno, miguu na mgongo nikawa siwezi hata kusimama
 lakini angalau sasa hivi naweza kusimama japo si kwa muda mrefu, 
nawashukuru sana watoa huduma wetu wa afya walijitahidi kutuhudumia” 
alisema Mhe. Consolata Lushu Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Wilaya
 ya Meatu.
Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu,Bw. 
Donald Magesa amesema jitihada kubwa zimefanyika katika kuokoa maisha 
yao tangu ajali ilipotokea na akawashukuru wote waliowahudumia kutoka 
Simiyu na Mwanza huku akiwawahakikishia kuwa Chama Cha Mapinduzi 
kitakuwa pamoja nao muda wote na wanawaombea madiwani wote wapone 
haraka.
Aidha, Magesa amesema Chama cha 
Mapinduzi kinaendelea kutoa pole kwa familia na ndugu wa Marehemu Mahega
 Masunga Selemani Diwani Kata ya Tindabuligi, ambaye alipoteza maisha 
katika ajali hiyo ambapo mwili wake unatarajiwa kuzikwa siku ya 
 Jumatano nyumbani kwao Kijijini Zebea Wilayani Maswa.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali 
ya Mkoa wa  Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka amemshukuru 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ambaye pia ni Mbunge wa 
Jimbo la Kisesa wilayani Meatu kwa kusaidia kukodi ndege maalum kwa 
ajili ya kuwasafirisha madiwani hao na akawatakia  safari njema na 
kuwaombea heri ili wapone haraka na kurejea kwenye kazi ya kuwatumikia 
wananchi.
Mtaka pia amewashukuru madaktari 
waliowahudumia majeruhi wote tangu siku ya ajali Juni 10, wa kituo cha 
Afya Mwandoya, Hospitali ya Wilaya ya Meatu, Hospitali Teule ya Mkoa na 
Hospitali ya Rufaa Bugando ambapo amebainisha kuwa kwa hali 
iliyoripotiwa wakati wa ajali kama kungetokea uzembe wowote kwa 
madaktari watu wengi wangepoteza maisha, lakini kutokana na wepes wao wa
 kutoa huduma wamesaidia kuokoa maisha ya waliojeruhiwa
Wakati huo huo Mtaka ametoa pole 
kwa familia ya Marehemu Mahega Masunga Selemani Diwani Kata ya 
Tindabuligi ambaye alipoteza maisha katika ajali hiyo na kuwahakikishia 
kuwa Serikali ya Mkoa itashiriki katika mazishi ya diwani huyo na 
kueleza kuwa Uongozi wa Mkoa uko pamoja na familia na Baraza la Madiwani
 wa Wilaya ya Meatu katika wakati huu mgumu.
Waheshimiwa Madiwani 
waliosafirishwa kweda Muhimbili ni Pius Machungwa Diwani wa Kata ya 
Ngh’oboko na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Emmanuel 
Mboje , Emmanuel Chalya, Seni Mizumale, Consolata Lushu, Juma Mpina, 
Chalya Igulu, Njile Ngwakwa, Mlangale Sakumi.na wengine wawili ambao ni 
Daudi Solo na Jeremia Kishola wamefanyiwa upasuaji Hospitali ya Rufaa 
Bugando na wapo katika vyumba vya uangalizi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni