Vigogo Zaidi ya 900 Kuchunguzwa Upya Mali Zao Wanazomiliki




Image result for Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela





Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela amesema tayari wamechagua viongozi 946 kwa ajili ya kuanza kufanya uhakiki wa mali za viongozi hao ili kuthibitisha thamani na uhalisia wa mali hizo na kutambua namna walivyozipata.
Amesema kuwa zoezi hlo linatarajiwa kufanyika ndani ya mwezi mmoja kuanzia Juni 18 hadi Julai 18 mwaka huu.
Uhakiki huo unatarajiwa kufanyika kwa baadhi ya viongozi na si viongozi wote ,sababu ikiwa ni kutokana na Serikali kutokuwa na fedha za kutosha za kuhakiki viongozi wengi kwa wakati mmoja.
Amesema lengo la uhakiki huo ni kuthibitisha uhalisia wa mali hizo, kulinganisha na tamko la rasilimali na madeni.
"Hili ni jambo la kisheria si kwamba tunahakiki kwa kumtuhumu kiongozi yeyote na zoezi hili litawafikia wote lazima wahakikiwe,” amesema.
Amesema maofisa wa sekretarieti watahitaji kuona nyaraka za mali husika ambazo zimeainishwa kwenye tamko.
"Tutaanza Juni 18 hadi julai 18, watumishi wa sekretarieti watawafuata viongozi hao na kuwahakiki. Tunachoomba kwa viongozi wawape ushirikiano na kulifanya zoezi hili kuwa rahisi kwa kuwaandalia nyaraka husika," amesema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni