Mahmoud Ahmad, Arusha
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Meru mkoani Arusha imepanda miti 7000 huku miti 500
ikipandwa katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani pamoja na kuweka
bikoni katika mipaka inayozunguka vyanzo vya maji.
Juni
tano ya kila mwaka huwa ni Siku ya Mazingira Duniani ambapo wadau
mbalimbali huitumika kufanya kampeni na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa
kutunza mazingira.
Akizungumza
wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani Ofisa
Mifugo Wilaya ya Meru Dk. Amani Sanga kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo
amesema kuwa Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi Barani Afrika na
duniani imeendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa
mazingira unaotokana na shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo, ufugaji
na ujenzi.
Amesema
kauli mbiu kwenye siku hiyo kwa mwaka huu inasema hivi "Mkaa ni gharama
tumia nishati mbadala" ambapo ameifafanua inamaanisha jamii kuwa na
urafiki endelevu na mazingira asilia.Kila mtu anapaswa kutambua,
kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira asilia na
kuhamasishana ili kuyatunza na kuyahifadhi.
"Uharibifu
huu wa misitu hutokana na shughuli za kilimo na ufugaji kwa njia zisizo
endelevu. Uharibifu huu wa misitu unachangia pia kukosekana kwa mvua,
kukauka kwa mito, mabwawa na uoto wa asili,"amesema .Amebainisha
kazi ya kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi
mazingira inahitaji ushirikiano wa wadau katika ngazi zote na si jukumu
la Serikali peke yake.
Dk.Sanga
ameongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru katika kuazimisha siku hiyo
imepata ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo Bonde la
pangani, mMali hai klabu,Kili flora, Mamlaka ya making mjimdogo wa uUsa
River Pamoja na SUAMA.
Hivyo
amesema taasisi na asasi za kiraia zikishirikiana katika kutekeleza
kikamilifu sheria na kanuni za uhifadhi wa mazingira nchini itasaidia
kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.Kwa
upande wa Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Bonde la pangani Abraham Yesaya
amesema kuwa jumla ya miti 7000 imepandwa katika kata 12 na kutoa elimu
ya misitu katika shule zaidi ya 20.
Amesisitiza
ni wajibu wa mamlaka katika ngazi mbalimbali ziwe na mipango bora ya
ardhi, mikakati ya uhifadhi wa vyanzo vya maji, pamoja na udhibiti wa
uvunaji holela wa misitu na ufugaji usio endelevu.Pia
kutoa elimu juu umuhimu wa kutunza mazingira na faida zinazopatikana
ili wananchi waunge mkono jitihada zinazofanywa katika kulinda na
kuhifandhi mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngyani kilichopo katika kata ya Nkwaranga
katika halmashauri hiyo Elishilia Mathayo amesema amefurahishwa na hatua
ya kuwekwa bikoni katika mipaka ya vyanzo vya maji kwani hiyo itasaidia
kuongeza ulinzi na watu kutoharibu vyanzo hivyo.
"Bikoni
hizi zitasaidia kuonesha wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu
kutambua mipaka yao ya kufanya shughuli bila kuingia kwenye vyanzo vya
maji ambavyo vinastahili kulindwa na kila mmoja wetu,"amesema.
Afisa
mifugo wa Meru Dkt. Amani Sanga akizungumza katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani na wananchi wa kijiji cha
Ngyani kilichopo katika kata ya Nkwaranga ndani ya halmashauri ya Meru .
Afisa
Maendeleo ya Jamii wa bonde la pangani Abraham Yesaya akiwa anaelezea
shughuli ambazo wanazifanya wao kama bonge la pangani
Mgeni rasmi akipanda moja ya miti
Baadhi ya wadau wa SUAMA wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi mara baada ya kufanya shughuli ya upandaji miti
Mwenyekiti
wa kijiji cha Ngyani kilichopo katika kata ya Nkwaranga katika
halmashauri ya Meru, Elishilia Mathayo akizungumza katika maadhimisho
hayo
mmoja
wa wananchi ambaye jina lake halikufahamika akitoa dukuduku lake mbele
ya mgeni rasmi ambapo aliomba zoezi hili la upandaji miti liwe endelevu
mbali
na upandaji miti pamoja na uelimishaji juu ya utunzaji wa mazingira pia
halmashauri ya meru kwa kushirikiana na bonde la pangani waliandaa
maonyesho ya majiko mbalimbali ambayo yanatunza mazingira kama kauli
mbiu inavyosema mkaa ni gharama tumia nishati mbadala
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni