Watumishi sita bodi ya mikopo watumbuliwa






Bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewasimamisha kazi watumishi wake sita kwa makosa mbalimbali ya kuisababishia serikali hasara ya mabilioni ya fedha kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi Abdulzack Badru leo Juni 13 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kuwataja viongozi hao kuwa ni Juma Hamisi Chagonja Mkurugenzi wa urejeshaji wa mikopo aliye sababisha hasara kwa uzembe na kushindwa kutumia majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa sheria.

Wengine ni Onesmo Ngitiri Laizer Mkurugenzi upangaji na ugawaji mikopo ambaye amesababisha hasara ya bilioni 7.1, John Elius Mkurugenzi msaidizi ugawaji mikopo hasara ya bilioni 7.1, Bwana Robert Kibona Mkurugenzi msaidizi wa urejeshaji mikopo, Bwana Heti Sago Mkaguz mkuu wa ndani wa hesabu, na Bwana Chikira Habari Mkurugenzi msaidizi wa upangaji mikopo hasara ya Bilioni 7.1.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni