NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI imesema haitasita kuzifuta na kuzinyang’anya leseni Kampuni ambazo zinanua pamba hapa nchini ikiwa zitachelewesha fedha za wakulima wa zao hilo na kuanza kuwazungusha bila kuwalipa fedha zao.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba wakati akizindua ununuzi wa Pamba katika Kijiji cha Muhilidede wilayani Uyui Mkoani Tabora
Alisema ni jukumu la Kampuni zinapomaliza kununua pamba ya mkulima kumlipa palepale siku hiyo hiyo kwa kuwekea fedha katika Akaunti yake au kupitia simu ya mkononi na kisha pesa ikishaingia anaone ujumbe wa kumhakikisha kulipwa
Waziri huyo aliwataka Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika, Halmashauri za Wilaya na Wakulima walisikubali Kampuni ziondoe pamba katika Vituo vya kununulia pamaba kama malipo kwa wakulima hajafanyika na chama cha mshingi na Halmashauri hazijalipwa.
Dkt. Tizeba alisema Serikali inaachukua hatua hiyo ili kurejesha imani kwa wakulima juu ya ushirika ambao umekuwa ukipigwa vita na baadhi ya watu.
Aidha Waziri huyo aliwaagiza Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika kuhakikisha vinawakamata na kuwapeleka Polisi watu wote ambao watapeleka pamba iliyochanganywa na uchafu na ile wekewa maji kwa sababu watu hao ni sawa na wezi.
Alisema mkulima anaweka maji kwenye pamba na yule anayeweka uchafu anataka kuhujumu zao hilo kwa kusababisha mbegu zitakazolishwa zisiote na wanunuzi watoe bei mbaya kwa pamba chafu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliwataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kutumia sehemu ya asilimia 33 ya kila kilo watakayopata kununua Matrekta ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo msimu ujao.
Alisema kuwa kupitia kilimo cha matumizi ya jembe la mkono hakiwezi kuleta mapinduzi ya kilimo na manufaa kwa mkulima mkoani humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni