“PAMBA ISITOKE KIJIJINI KABLA MKULIMA KULIPWA FEDHA ZAKE” DKT TIZEBA


Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mulidede kilichopo Kata ya Shitage Wilayani Uyui akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora, Picha Zote Na Mathias Canal, WK. Leo 11 Juni 2018.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akishuhudia zoezi la uuzaji na ununuzi wa pamba katika kijiji cha Ishihimulua kilichopo Kata ya Bukumbi Wilayani Uyui akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mulidede kilichopo Kata ya Shitage Wilayani Uyui akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.
Wakazi wa kijiji cha Mulidede kilichopo Kata ya Shitage Wilayani Uyui wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji na kata ya Miguwa Wilayani Nzega akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Tabora.
 
Na Mathias Canal,
WK-Tabora
 
Waziri wa kilimo Mhe
Dkt Charles Tizeba amepiga marufuku kwa wanunuzi wa pamba kuondosha pamba ya
wakulima kwa maelewano ya kulipa baada ya siku kadhaa badala yake ameagiza
wakulima wa pamba kulipwa fedha zao kabla ya pamba kusafirishwa.
 
Dkt Tizeba amepiga
marufuku hiyo akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Tabora leo 11
Juni 2018 wakati akihutubia wakulima wa pamba katika kijiji cha Mulidede na
Ishihimulua vilivyopo katika Wilaya ya Uyui sambamba na kijiji cha Miguwa
kilichopo katika Wilaya ya Nzega.
 
Dkt Tizeba alisema kuwa
kumekuwa na ombwe la wakulima kucheleweshewa malipo yao baada ya kupeleka pamba
kwenye kampuni za ununuzi jambo ambalo linachelewesha upatikanaji wa huduma za
kijamii kwa wakulima hao na familia zao kwa ujumla kwa wakati tarajiwa.
 
Alisisitiza kuwa ili
pamba iweze kusafirishwa kwenda popote baada ya mauziano ni lazima mkulimwa
alipwe stahiki zake kwa wakati sio kuishi kwa kukopesha bidhaa hiyo muhimu
isiyokuwa na uduni wa soko.
 
Dkt Tizeba amemaliza ziara
ya kikazi katika Mkoa wa Tabora akitokea mkoa wa Singida ambapo pamoja na mambo
mengine anakutana na wakulima na wanunuzi wa pamba ili kujionea zoezi la
ununuzi na uuzaji wa pamba.
 
“Lakini ndugu zangu
wakulima na ninyi ni lazima niwaambie ukweli baada ya kuuza pamba mnapaswa kuwa
makini katika matumizi ya fedha zenu kwani endapo mkitumia hovyo vile vile
fedha hizo zitamalizika pasina kufanya jambo la maendeleo kwa familia na jamii
kwa ujumla” Alikaririwa Dkt Tizeba
 
Katika hatua nyingine
Dkt Tizeba ametangaza neema kwa wakulima wa pamba kwa kuwafahamisha kuwa kila
mwananchi aliyelima pamba ni mwanachama wa chama cha ushirika AMKOS hivyo ana
sifa za kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha ushirika.
 
Tayari waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba amewasili Wilayani Kahama ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa masoko ya Tumbaku Kitaifa hafla itakayofanyika katika mkoa wa kitumbaku-Kahama 12 Juni 2018.
 
MWISHO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni