MKUTANO  wa kihistoria kati ya 
Rais wa Marekani,  Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini,  Kim 
Jong Un,  umefanyika nchini Singapore.
Wawili hao walikutana kwanza kwa 
dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili  
pekee yao na wakalimani wao.
Mkutano huo ulianza kwa viongozi  
hao wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba 
ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana
 baina yao.
Rais Trump amesema wawili hao wamepiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka za makubaliano.
Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia
 za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na
 Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.
Hata hivyo, haijabainika ni nini 
kitakuwepo kwenye waraka ambao watautia saini. Trump alisikika akisema 
kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa 
haikuwa rahisi kufika hapo.
Mkutano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu naulifanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.
Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.
Baadaye washauri na maofisa 
mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la 
nyuklia likitarajiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado 
makubaliano yatakuwa yapi.  Akizungumza kabla ya mkutano, Katibu Mkuu wa
 Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres,  amesema kuwa umoja huo utatoa 
msaada wowote wa kuhamasisha makubaliano katika mkutano huo.
”Viongozi wawili, wanajaribu 
kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata 
mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndiyo vinabaki kuwa 
lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kwamba kutahitajika 
ushirikiano wa hali ya juu na kutakuwa na changamoto za hapa na pale 
katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote hali 
hiyo,” alisema Guterres.
Mkutano huu unaweza kuwa na 
mafanikio Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na 
mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na 
kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua
 wawili hao kukutana.
Kwa nini hatua hii imefikiwa hivi sasa?
Mwaka wa kwanza wa Trump katika 
kiti cha urais ulianza kwa mvutano mkubwa na kurushiana maneno huku Kim 
naye akiendeleza majaribio ya silaha za nyuklia na kukiuka ilani ya 
kimataifa. Rais wa Marekani aliapa kupambana ikiwa Pyongyang ingeendelea
 kuitishia Marekani.
Korea Kaskazini iliendelea kukaidi na kufanya jaribio la nyuklia la sita mwezi Septemba mwaka 2017.
Baadaye Kim alitangaza kuwa nchi 
yake imefanikiwa katika mpango wake wa kuwa taifa la nyuklia, likiwa na 
silaha zinazoweza kuifikia Marekani.
Lakini mwanzoni mwa mwaka 2018, 
Korea Kaskazini ilianza kuboresha mahusiano na Korea Kusini kwa kupeleka
 timu na ujumbe kwenye michuano ya Olimpiki mjini Pyongyang.
Mwezi Machi, Donald Trump aliushangaza ulimwengu kwa kukubali mwaliko kutoka kwa Kim wa kukutana ana kwa ana.
Tangu wakati huo, njia ya kuelekea
 mkutano huu ikawa yenye changamoto ambapo Trump alikuwa akiahirisha 
kila mara kukutana huko.   Lakini hatimaye viongozi hao wamekaa pamoja. 
Singapore ni nchi ya tatu ambayo Kim Jong-un ameitembelea tangu 
alipokuwa kiongozi wa nchi yake mwaka 2011.
Safari yake ya kwanza ilikuwa 
nchini China mwezi Machi na mwezi Aprili akawa kiongozi wa kwanza wa 
Korea Kaskazini kutembelea Korea Kusini ambapo alikutana na Moon Jae-in.












Hakuna maoni:
Chapisha Maoni