Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza na waandishi wa habari
katika kampeni maalumu ya kuzuia uharibifu wa miundombinu ya umeme
mkoani humo.
Meneja
wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka
akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi
inayoendelea mjini Moshi
Meneja
wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka
akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi
ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika
hilo Salama
Meneja
wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka
akiwaonyesha waandishi wa habari ambao hawapo pichani baadhi ya miradi
ya umeme inayoendelea mjini Moshi pembeni ni Afisa Uhusiano wa Shirika
hilo Salama.
Mafundi wa Tanesco wakikata miti iliyopita katika njia za umeme Moshi.
Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Bi Anna Mghwira ametoa onyo kali kwa wakazi wa
mkoa huo wanao jihusisha na uhabifu wa miundombinu ya Shirka la Umeme
Tanzania (Tanesco) na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema, serikali inatumia gharama kubwa sana kuendesha
shirika hilo hivyo kulihujumu kwa kuharibu miundimbinu sio sahihi na
halivumiliki.
Aliyasema
hayo jana wakati akiongea na waandisi wa habari, katika kampeni maalumu
inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha juu ya
athari za kuhujumu miumbombinu ya shirika hilo.
“Hivi
karibuni kumekuwepo na matukio ya baadhi ya watu kupoteza maisha baada
ya kujaribu kujiunganishia umeme kwa njia ya wizi. naagiza wakazi wa
mkoa huu kuacha kabisa tabia hiyo kwani matukio ya aina hiyo ni sawa na
matukio ya uhujumu uchumi, ambayo yanarudisha nyuma jitihada za Serikali
za kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana na hivyo kufikia uchumi wa
kati kupita viwanda,” alisema
Aliongeza
kuwa uhujumu wa miundombinu sio tu inaleta hasara kwa shirika lakini
pia inapelekea kupoteza nguvu kazi ya taifa kupitia maafa mbalimbali
ikiwemo vifo na ulemavu kwa watu wanaohusika na matukio hayo. Naye
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kilimanjaro Mahawa Mkaka alisema changamoto
ya uharibifiu wa miumbombinu unatokana na uelewa mdogo kuhusiana na
madhara yatokanayo na umeme.
Pamoja
na hayo shirika katika mkoa linajitahidi kufanya uhamasishaji wenye
lengo la kuelemisha watu kujiepusha na uharibifu wa miundombinu.
“Tunatoa
rai kwa wakazi wa mkoa huu kuwa madhalani wanataka kukata miti ambayo
ipo karibu ya nyaya za Tanesco watoe taarifa ili wataalamu wetu wasaidie
kwenye zoezi kwa kinyume na hapo wanaweza kupata matatizo ikiwemo
kifo,” alisema meneja
Alisema
kwa mwaka jana zaidi ya ajali zipatazo 30 ikiwepo ajali za moto na watu
kupoteza maisha kutokana na matukio mbalimbali, “Nia ya shirika ni
kuona tunamaliza mwaka bila ajali hata moja inayotokana na umeme,” Aidha,
maneja alisema kwa mwaka mkoa unapoteza asilimia mbili ya mapato
yanayotokana na wizi wa umeme na uharibifu wa miundombinu ambapo fedha
hizo zingetumika kuboresha zaidi upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Maneja
huyo amewaomba wakazi wa mkoa huo kuendelea kushirikiana na shirika ili
kuwabahini wanaoendeleza vitenda vya wizi na uharibifu. Alisema
mwaka jana pekee zaidi ya Sh50 milioni zilipatikana kutoka na faini
mbalimbali zinazotokana na uharibifu wa miundombinu.(Habari kwa Hisani
ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni