KAYA MASIKINI 90,720 MKOANI TABORA KUNUFAIKA NA MAJIKO BANIFU


1a
Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Valentine Msusa  wakati akitoa ufafanuzi jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye shati  jeupe) matumizi ya majiko banifu waliopatiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia TFS kwa ajili ya kaya masikini.
2
Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Valentine Msusa  wakati akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye shati  jeupe) na Wakuu wa Wilaya za Tabora moja ya jiko banifu waliopatiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia TFS kwa ajili ya kaya masikini  wakati wa makabidhiano jana mjini Tabora.
3
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) na  Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Valentine Msusa (kushoto) wakiwa wameshika moja ya jiko banifu waliopatiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia TFS kwa ajili ya kaya masikini mkoani humo jana wakati wa makabidhiano.
4
Baadhi ya vijana wakishusha majiko banifu 90,720 ambayo yametolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kusambazwa mkoani Tabora kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kwa ajili ya kaya masikini.
5
Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Valentine Msusa (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya upangaji wa majiko banifu waliopatiwa Mkoa wa Tabora na Mamlaka ya Mapato Tanzania kupitia TFS kwa ajili ya kaya masikini.
Picha na Tiganya Vincent
………………….
NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza  kuzisambazia kaya 90,720 Mkoani Tabora majiko banifu ambayo yatumia mkaa kidogo na kuni chache na hivyo kuepusha ukataji ovyo wa mistu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Valentine Msusa  wakati akikabidhi msaada majiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo.
Alisema majiko hayo ambayo yanatoka nje ya Nchi ni rafiki wa mazingira yanatarajiwa kusambazwa kwa kaya masikini mkoani Tabora kwa ajili ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuni kwa kaya hizo.
Msusa alisema majiko hayo ni rafiki wa mazingira na yakisambazwa kwa wingi yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.
Alitaja faida nyingine ni pamoja na majiko hayo ni rafiki kwa watumiaji wa kuni kuepuka kuingiliwa machoni na moshi wa miti ambayo wakati mwingine ina sumu.
Alitoa wito kwa Kampuni ambazo zinajihusisha na teknolojia ya utengenezaji wa majiko banifu kuangalia uwezekano wa kuja na aina hiyo ya majiko na kuzalisha kwa wingi ili jamii kubwa ya Watanzania iweze kuanza kutumia na hivyo kuokoa mistu hapa nchini.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa msaada huo ambao utasaidia kuunga mkono kampeni za Mkoa huo za kukabiliana na uharibifu wa mazingira na upandaji miti.
Alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuhakikisha wanaongeza jitihada ya kutengeneza majiko ambayo yatasaidia kupunguza uharibifu wa mistu unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya mkaa na kuni za kupikia.
Mwanri alitoa wito kwa wahusika kuharakisha kuyagawa majiko hayio kwa kaya masikini katika Halmashauri zote nane za Mkoa huo ili wahusika wapunguze matumizi ya mkaa na kuni.
Msaada huo ulitolewa na TRA baada ya wahusika kushindwa kulipa kodi na hivyo kutaifishwa na Serikali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni