Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akimkabidhi Bw. Leonard Kushoka mfano wa hundi yenye thamani ya
shiliningi za kitanzania milioni 300 mara baada ya kuibuka mshindi wa
shindano la teknolojia ya nishati mbadala wa mkaa mwaka 2018, wengine
pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. January Makamba na Mwenyekiti Mkazi wa Kampuni ya Shell Bw. Axel
Knospe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizindua ukuta uliojengwa kwenye kingo za Bahari ya Hindi pembezoni mwa
barabara ya Barack Obama leo kuli ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba na Mwenyekiti Mkazi wa
Kampuni ya Shell Bw. Axel Knospe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ukuta wa bahari
wenye urefu wa mita 920 uliojengwa pembezomi mwa barabara ya Barack
Obama mara baada ya kuizindua, mwingine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakati wa uzinduzi wa ukuta uliojengwa kwenye kingo za
Bahari ya Hindi pembezoni mwa barabara ya Barack Obama leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia uzinduzi wa
ukuta uliojengwa kwenye kingo za Bahari ya Hindi pembezoni mwa barabara
ya Barack Obama leo kulinda mazingira ya fukwe.
………………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa
ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati
na miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
Makamu wa Rais wa ameyasema hayo
wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo
kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.
“ Ni muhimu, mipango ya maendeleo
katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na
maendeleo endelevu” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema kazi ya
kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira unahitaji
ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote.
Maadhimisho ya Kimataifa
yanafanyika India katika mji wa New Delhi yakibeba ujumbe wa kuhimiza
kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za
plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa
maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati Mbadala”
Mapema leo, Makamu wa Rais
alizindua ukuta wa bahari uliopo kwenye barabara ya Barack Obama wenye
urefu wa mita 920, ukuta huo ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi
kavu unakadiriwa kuwa na maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa.
Makamu wa Rais amesema kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda na zipo
faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na Tanzania kuwa na
Viwanda.
Mwisho, Makamu wa Rais amesema
katika kufanikisha suala zima la uhifadhi wa Utunzaji wa mazingira mi
lazima tuifanye kila siku iwe siku ya Mazingira.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni