Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba wanawake wenye tabia ya
kuvaa sketi fupi maarufu Vimini na nguo za kubana wakati huu wa mfungo
wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan wakaacha kuzivaa katika kipindi hiki ili
kuhakikisha waumini wa dini ya Kiislamu wanatekeleza funga hiyo vema.
Makonda
ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anapokea msaada wa
tende kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi Darul Irshad Centre Islamic
Tanzania Arif Yusuf AbduRahman kwa kushirikiana na taasisi rafiki ya
Muraj Islamic Centre Tanzania.Makonda ameagiza tende hizo zipelekwe
katika vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Wakati
anazungumzia funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambayo waumini wa dini
ya Kiislamu wanaendelea nayo amesema ni vema waumini wa dini zote
wakashiriki katika kufanikisha waliofunga wanatekeleza moja ya nguzo za
dini hiyo vema.Hivyo amewaomba wanawake wenye tabia ya kuvaa vimini na
nguo za kubana katika mwezi huu wakaacha kuzivaa ili kutoa nafasi ya
waliofunga kutoingia majaribuni kutokana na mavazi hayo.
"Niwaombe
akina dada wanaopenda kuvaa nguo za kubana hasa vimini kuacha kuvaa
hadi hapo mfungo utakapokwisha.Natambua wananchi wa Mkoa wa Dar es Salam
wapo wenye imani tofauti lakini bado tunayo nafasi ya kuheshimi imani
ya kila mmoja wetu,"amefafanua Makonda.Pia ametoa ombi kwa
wafanyabishara kutopandisha bei ya vyakula katika kipindi ambacho
waumini wa dini ya Kiislamu wanaendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhan.
"Wananchi
wa Dar es Salaam niendelee kutoa ombi tuwape ushirikiano ndugu zetu
walioko kwenye funga na kwa wafanyabiashara msipandishe bei ya
vyakula,"amesisitiza.Kuhusu tende ambazo zimetolewa na taasisi hiyo
Makonda amesema zitakwenda kugawiwa vituo vya watoto yatima vilivyopo
Dar es Salaam na anaamini kwa kugawa tende hizo kwenye vituo hivyo ni
sehemu ya kuwakumbuka watoto walioko huko ambao wapo ambao wapo kwenye
funga.
Pia
ameishukuru Taasisi ya Darul Irshad Centre Islamic Tanzania kutokana na
namna inavyotoa misaada ya aina mbalimbali kwa wananchi wa Dar es Salaam
na siku za karibuni wametoa msaada wa magodoro 500 pamoja na vyakula
kwa ajili ya kuwasaidia waliokumbwa na mafuruko yalitokana na mvua za
masika.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Darul Irshad Centre Islamic Tanzania AbduRahman
amesema taasisi hiyo imesema lengo kubwa la taasisi hiyo ni kusaidia
jamii yenye uhitaji na kufafanua tende hizo ambazo wamekabidhi leo
zimetoka kwa wageni ambao wamekuwa wakija nchini kupitia taasisi hiyo na
moja ya mambo ambayo wamekuwa wakifanya wanaporudi kwao ni kusaidia
jamii yenye uhitaji.
Awali
kabla ya kufika kwa Makonda, AbduRahman ameelezea changamoto anayoipata
kwenye taasisi yake ambayo imekuwa ikipokea wageni ambao ni waumini wa
dini ya Kiislamu na lengo la kuja kwao nchini mbali ya kuzungumzia dini
wanasaidia wananchi.
Hata
hivyo amesema pamoja na wageni hao kuwa na vibali vya kuingia nchini
lakini bado wamekuwa wakisumbuliwa na baadhi ya maofisa wa uhamiaji na
kufafanua ujio wa wageni hao ni wenye nia njema na sehemu kubwa
umejikita katika kusaidia zaidi na ni watu wema.
Baadhi
ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Taasisi ya Darul Irshad Centre
Islamic Tanzania wakibeba tende kabla kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam leo
Baadhi
ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Taasisi ya Darul Irshad Centre
Islamic Tanzania wakibeba tende kabla kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam leo
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Darul Irshad Centre Islamic Tanzania AbduRahman leo jijini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni