UFUATILIAJI WA SHERIA NDIO TATIZO UTUNZAJI WA MAZINGIRA NCHINI


1549511_Articolo
Na Ahmed Mahmoud
Sheria mbali mbali zimekuwa zikitungwa kuhusiana na utunzaji wa mazingira lakini bado kumekuwa na ombwe la uharibifu na ukataji mkubwa wa misitu hapa nchini na kupelekea mabadiliko ya tabianchi je tatizo lipo wapi ni kwenye ufutaliaji wa sheria au elimu kwa wanchi haijawafikia.
Utaona pindi yanapotokea majanga mbali mbali hapa nchini ndipo kauli mbali mbali zinatoka mifano ipo mingi yakiwemo magonjwa ya milipuko mafuriko bila kuandaa mazingira yetu kabla ya kuharibika suala hili ndio chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira hapa nchini.
Tarehe 5 ya mwezi wa sita  kila mwaka duniani kote husherehekea siku ya mazingira Duniani na nchini siku hiyo husherehekewa kwa upandaji wa miti na utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira sanjari na matamasha,maonyesho na mikutano ya hadhara lengo kuu ni kufikisha ujumbe wa siku hiyo.
Sote ni muhimu kutambua kuadhimishwa kwa siku hii ya mazingira duniani kwani siku ya mazingira duniani ni siku iliyopangwa kimataifa ili kutoa fursa ya kukuza uelewa wa jamii na kuchukuwa hatua za maksudi za kuhifadhi na kutunza mazingira kwa ustawi wa maisha ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Tatizo la uharibifu wa mazingira ni la ulimwengu wote ambalo linatokana na kuongezeka kwa shughuli mbali mbali za kimaendeleo katika Nyanja za kiuchumi na kijamii ambazo zimesababisha uchafuzi wa mazingira na kuathiri maisha ya mwanadamu na viumbe vingine.
Hali hii ya uchafuzi wa mazingira imesababisha majanga mbali mbali ya kimazingira na kijamii kama mafuriko na kuenea kwa hali ya jangwa ambayo ni matokeo ya mabadiliko ya tabianchi.
Matokeo haya yanasababishwa na binadamu hasa mataifa yalioendelea kiuchumi yanapofanya shughuli za kiuchumi na maendeleo bila kuwaza matokeo ya shughuli hizo kwenye mazingira na uharibifu wake.
Aidha  Afisa mazingira jiji la Dodoma Ally Mfinanga Kujisahau kwetu ndio kumetufanya binadamu kuwa waathirika wa mafanikio yetu mwenyewe(the victim of his own succer’) na dunia inalia kwa sababu ya madhara yaliojitokeza baada ya mwanadamu kujitenga na mazingira.
Amesema kuwa Uchafuzi huu unatokana na mambo makuu mawili,uzalishaji wa taka unaozidi uwezo wa mazingira kuhimili taka hizo hasa taka za plastiki jambo hili linahusisha kauli mbiu ya kimataifa ya mwaka huu inayosema kuwa
“ pambana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka hasa za plastic’’ hii itaondoa tatizo lilopo la kuteketeza taka ngumu zilizoenea katika makazi yetu” alisema Mfinanga
Taka hizi za Plastiki zimekuwa ni kero kubwa ya uharibifu wa mazingira katika jamii nyingi  zinazozalisha taka hizi zina madhara mbali mbali ya kijamii na kimazingira kama ifuatavyo “uharibifu wa hewa(dioxine anda furans)unatokakana na kuunguzwa kwa plastik’
Uchafuzi wa vyanzo vya maji kama vile mito maziwa na bahari ambapo taka hizi huathiri mazalia ya viumbe wa majini hususani samaki na kuhatarisha maisha ya wanyama wanapokula plastiki hufa.
Taka hizi pia huharibu miundo mbinu ya maji mfano  mabomba na mifereji ya kupitishi maji kwa kusababisha kuziba hali hii ni moja ya uharibufu wa mazingira,kuharibu muonekano wa mazingira hasa maeneo ya wazi na kando kando ya barabara.
Narudia Kauli mbiu ya kitaifa  mwaka huu “mkaa ni gharama tumia nishati mbadala” utaona matumizi ya mkaa ndio imekuwa nishati mbadala hapa nchini huku wataalamu wakitoa nasaha mbali mbali yakupunguza matumizi ya nishati hiyo.
Kama tutachukuwa hatua za maksudi kuhakikisha tunabadili mwelekeo wa matumizi ya mkaa na kuangalia nishati mbadala tutaepuka na kuiepusha nchi kuingia katika mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na shughuli zetu za kiuchumi.
Siku hii hapa nchini kitaifa ilifanyika jijini Dar es salaam na mkoani Dodoma yalipo makao makuu ya nchi yalifanyika kwenye viwanja vya Nyerere ambapo mgeni Rasmi alikuwa Naibu Meya wa Jiji Hilo Jumanne Ngede ambaye aliwataka watumishi wa halmashauri hapa nchini kuanza kujitathimini kama wamefikia malengo ya serikali katika suala zima la utunzaji wa mazingira katika halmashauri zao.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi  wa jiji la Dodoma Dickson Kimaro ambaye ni Afisa mazingira wa jiji hilo anasema kuwa wamejipanga kuhakikisha Sheria zinafuatwa na watakaobainika wanavunja sheria hatua kali zitachukuliwa iliwamo faini ya 50,000 au kupandishwa mahakamani au vyote kwa pamoja.
Amesema kuwa matumizi ya rasilimali za kimazingira kupita uwezo wake kujirejeza jambo hilolinahusisha kauli mbiu ya kitafa inayotanabaisha kuwa mkaa gharama tumia nishati mbadala ambayo itaokoa uharibifu wa misitu yetu.
Amesema kuwa ilimu wataendeleo kuitoa na kuwa atakaye mpeleka mtuhumiwa wa uchafuzi na uharibifu wa mazingira tapewa asilimia 50% ya fedha ya faini na kuwataka wananchi pamoja na askari jamii kuhakikisha watandea kazi hiyo kwa uweledi.
Kutokana na kauli hiyo ya Mh.Ngede inatukumbusha kwamba mahitaji yetu ya msingi yanatokana na rasilimali zilizoko kwenye mazingira ikihusisha hitaji muhimu la nishati ya kuni\mkaa ambazo zinatumiwa na wananchi wengi katika maeneo ya mjini na vijijini.
Hapa tunaona miti ni rasilimali muhimu sana kwa uhai na ustawi wa mwanadamu maana inahifadhi vyanzo vya maji na kusafisha hewa tunayovuta ili tuendelee kupata maji na kuvta hewa safi tunahitaji utunzaji wa misitu.
Hapa nchini kumekuwepo na ufyekaji wa uoto hasa misitu uliopitiliza uwezo wake wa kujirejeleza na matokeo tunetengeneza mazingira ya kuenea kwa hali ya jangwa hasa maeneo mbali mbali ambayo hapo awali yalikuwa ni vyanzo vikubwa vya maji.
 Muhimu elimu ikatolewa kwa jamii juu ua umuhimu wa hifadhi ya isitu ambao kazi yake kubwa ni kufyonza hewa ya ukaa(green house gas) ambayo ni chanzo kikuu cha mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira.
Rai yangu kwamba sote kwa pamoja tuwajibike kupanda na kutunza miti tutumie nishati mbadala na kuhakikisha taka zinatupwa katika hali iliyo salama kiafya na kimazingira ili vizazi vijavyo virithi hali tuliyoikuta sisi
Kama taifa sheria ziwekewe mkazo kama kwenye Halmashauri ya manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro walivyofanikiwa kuweka mji wao katika hali ya usafi na iwe tabia yetu isiwe nguvu ya soda mpaka kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni