Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
 Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuzungumza na 
wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
*****************
Na Emmanuel J. Shilatu
Rais wa Zimbabwe, Emerson 
Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe 
Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye 
maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. 
…
…
*Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa.
Mathalani, katika eneo la biashara
 kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara 
kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 
biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1.
*Pili*; *kushirikiana* vyema 
kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama 
vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima 
Kilimanjaro.
*Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha
 eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza 
lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo ajira
 nyingi za Waalimu na Madaktari zitazalishwa.
Rais wa Zimbabwe, Emerson 
Mnangagwa amewasili nchini Tanzania Alhamis Juni 28, 2018 kwa ziara ya 
kikazi na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe 
Magufuli.
Hayo ndio matunda ya Tanzania kuimarika kwenye mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo, matunda ya ziara ya Rais wa Zimbabwe nchini Tanzania.
Hayo ndio matunda ya Tanzania kuimarika kwenye mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo, matunda ya ziara ya Rais wa Zimbabwe nchini Tanzania.
Pongezi kwa Rais Magufuli na Rais Mnangagwa kwa kujenga historia mpya.
*Shilatu E.J*
0767488622
0767488622

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni