Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia,
Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA),
Mohamed Shabani (wapili kulia) akimkabidhi Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye tuzo ya cheti cha heshima, kwa
mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo
imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akionesha zawadi ya fulana ya
mabalozi wa Taasisi ya Salama Salimini aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa
Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo
Tanzania (AWAMATA), Mohamed Shabani (kushoto), kama alama ya kutambua
mchango wao katika kupambana na majanga ya moto na uokoaji, (kulia) ni
balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara. Hafla hiyo imefanyika Makao
Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, akifafanua jambo kwa Waandishi
wa habari (hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti cha
heshima kutoka kwa Idara ya Jinsia, Wazee na Watoto wa Asasi ya
Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), kwa mchango wao katika
kupambana na majanga ya moto na uokoaji. Hafla hiyo imefanyika Makao
Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (wa tatu kulia) akiwa na Viongozi
Waandamizi wa Jeshi pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia, Wazee na
Watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA), Mohamed
Shabani (wapili kushoto), (kulia) Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo
Billy Mwakatage, (kushoto) Kamishna wa Usalama Dhidi ya moto Jesuald
Ikonko na (wapili kulia) ni balozi wa Salama Salimini Mwinyi Mangara.
Hafla hiyo imefanyika Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji
…………….
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
limepokea tuzo ya cheti cha heshima kwa kutambua mchango wao katika
kupambana na majanga ya moto na uokoaji hapa nchini kutoka katika
Taasisi ya Wazalendo na Maendeleo. Tuzo hiyo imepokelewa na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye Makao Makuu
ya Jeshi hilo yaliyopo Dar es salaam
Akizungumza Kamishna Jenerali
baada ya kupokea tuzo ya cheti hicho. Alisema, anawashukuru Taasisi hiyo
kwa kulipa Jeshi hilo tuzo hiyo kwa kazi nyingi ambazo taasisi hiyo
imezifanya kwa kushirikia na Jeshi hilo ikiwepo kampeni ya kuitangaza
namba ya simu ya dharura 114.
Kamishna Jenerali Andengenye,
amezitaka Taasisi nyingine kushirikiana na Jeshi hilo katika kuzifufua
Fire Hydrant zilizo haribika na zilizofukiwa ili kuongeza idadi ya vifaa
hivyo ambayo ni msaada mkubwa wakati wa majanga ya moto. ‘‘Jamii
ishirikiane na Jeshi letu katika kuvilinda visima hivyo (Fire Hydrant) vilivyopo mitaani kwani ni msaada mkubwa pale majanga ya moto yanapotokea’’.
Ni vema sasa mamlaka
zinazoshughulikia miundombinu ya maji safi kwenye miji na majiji
ikazingatia wanapotengeneza miundo mbinu hiyo, wakumbuke kuweka na
mifumo ya maji ya zimamoto Fire Hydrant, pamoja na kuhakikisha wamiliki
wanaojenga majengo makubwa na madogo wanaweka mifumo hiyo ya maji.
Tuna changamoto kubwa kwa upande
wa visima hivyo, kwa hiyo kamapeni yetu ya kufufua na kuongeza visima
hivyo vitasaidia kuleta tija katika utendaji kazi katika fani yetu.
Tunashirikiana na Mamlaka za Maji kuhakikisha miundo mbinu hiyo inarudi
na kutoa ushauri pale miradi mipya ya maji inapo jengwa.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya
Wazalendo na Maendeleo Tanzania Bw. Muhammad Shaban alisema wamechukua
uamuzi huo wa kutoa Tuzo hiyo kutokana na kuona mchango mkubwa wa Jeshi
hilo walioutoa katika jamii. Pia amesema wataendea kutoa ushirikiano na
Jeshi hilo katika utoaji elimu kwa umma. “Tupo tayari kushirikiana na
Jeshi hili kuwaonesha sehemu zote ambazo fire hydrant zilizopo Mkoa wa
Dar es salaam.”
“Kampeni ya kufufua fire hydrant
imetugusa sana na kuona hatua hiyo ni msaada mkubwa kwa jamii kwani
zitasaidia magari ya zimamoto na uokoaji kupata maji eneo la karibu
majanga ya moto yanapotokea.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni