KAGERE,WAWA NA DIDA WATAMBULISHWA SIMBA


 
Klabu ya Simba imewatambulisha rasmi wachezaji wake wapya iliowasajili wiki hii mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam.
A
Wachezaji hao ni pamoja na beki Pascal Wawa aliyewahi kuichezea Azam FC, Mlinda Mlango Deogratius Munish ‘Dida’ ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga pamoja na Meddie Kagere kutoka Gor Mahia FC.
index
Kagere amekabidhiwa jezi namba jezi namba 14, Dida akipewa jezi namba 32 na Wawa akikabidhiwa namba 27.
36283360_1623993374395982_6927408152501551104_n
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameshindwa kuweka wazi juu ya mikataba waliyoingia na klabu lakini ikielezwa kuwa wamesaini miaka miwili kwa kila mmoja.
Baada ya utambulisho huo, Manara amefunguka na kueleza klabu imedhamiria kufanya usajili wa wachezaji hao ili kukipa nguvu kikosi cha Simba kwa ajili ya mashindano mengi ambao inakabiliwa nayo siku za usoni.
Kauli hiyo ya Manara imekuja kufuatia baadhi ya mashabiki na wadau wa soka kuhoji kwanini Simba inasajili wachezaji wengi na walioenda umri, lakini Manara amewakingia kifua kwa kueleza wana maana pana kufanya hivyo.
Manara ameeleza Simba itakuwa inakabiliwa na mashindano mengi hivyo inawapasa kuwa na kikosi kipana zaidi ukizingatia na ligi ijayo itakuwa na mechi nyingi kutokana na timu kuwa ishirini tofauti na mwanzo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni