AJALI YA NOAH YAUA WATANO MTWARA


IMG-20180628-WA0010

Muonekano wa gari aina ya Noah iliyokuwa ikufanya safari
zake kutoka Manganka kwenda Tunduru baada ya kuungua na kuteketea.
IMG-20180628-WA0014
Baadhi ya wananchii wa kijiji cha Chingweje wilaya ya
nanyumbu Mkoa wa Mtwara wakitazama Gari aina ya NOAH mara baada ya kugonga gema
la barabara na Kupinduka kisha kuwaka moto na kusababaisha watu watano
kufariki.
………………..
JOSEPH MPANGALA- MTWARA
Watu watano wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu kujerehiwa Vibaya
kutokana na ajali ya gari kuacha barabara Kuanguka na kisha Kuwaka moto
katika barabara ya Mangaka/Tunduru kijiji cha chigweje Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 10jioni ikihusisha gari aina ya Toyota Noah yenye namba  za usajili T.485 DJEiliyokuwa ikifanya safari zake kutoka Mangaka kwenda Tunduru ambapo Gari hiyo iligonga Gema na kupinduka eneo Lumesule ambalo lina kona na

mteremko mkali.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amesema Jumla ya watu watano wameungua mmoja ni dereva wa gari lakini wengine wanne hawajatambulika hivyo kuwaomba wananchii kujitokeza na kwenda kuwatambua Ndugu zao.

“Tunaomba wananchi wanaohisi kupotelewa na ndugu zao ambao walikuwa wanatambua kwamba nduguzao janawalikuwa na safari ya kutoka mangaka kwenda Tunduru na kama hawajafika nyumbani basi waende Hospital ya Mkoamaindo wilaya ya masasi kwa ajili

ya kutazama miili yao.Amesema kamanda Mkondya.

Aidha Kondakta wa gari hiyo Khalid Maneno aliruka kutoka kwenye gari hiyo kabla ya

kutokea ajali na hivyo anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa lengo lakusaidia kukamilisha Upelelezi
Uchunguzi wa awali unaonesha kuwachanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva na kutokana na mteremko na kona kali na hivyo kushindwa kuimudu na kupelekea ajali hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni