Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji  Wananchi
 Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 9 18, 2018. (Picha na
 Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, 
Jinana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza kabla ya 
kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Kongamano la Tatu la 
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 
18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
 baadhi ya viongozi walioshiriki katika Ufunguzi wa Kongamano la Tatu la
 Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakipiga makaofi baada ya Waziri Mkuu 
kufungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 
2018. kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, 
Faustine Kamuzora, Meya wa jiji la Dodoma,Profesa Davis Mwamfupe, Mkuu 
wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, 
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, 
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John
 Jingu, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Katibu Mtendaji
 wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa. (Picha
 na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
akimkabidhi Mhandisi, Salome Kabunda  kutoka TANROADS  Tuzo ya 
Uwezeshaji Kiuchumi, baada ya TANROADS kuibuka mshindi wa kwanza katika 
kundi la Wizara, Wakala na Idara za Serikali kwenye  Kongamano la Tatu 
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofunguliwa na Waziri Mkuu katika 
ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa 
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu. (Picha
 na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa 
kizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mku, Sera, Bunge, Kazi, 
Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  (katikati) Katibu Mkuu 
Ofisi ya Waziri Mku, Profesa Faustine Kamuzora baada ya kufungua 
Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye 
ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri 
Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
akizinduaTaarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi 
Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada ya kufungua Kongamano la Tatu
 la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF 
jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri 
Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama 
na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi 
Kiuchumi, Dkt. John Jingu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 
akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi
 Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada ya kuizindua  katika 
Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye 
ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, 
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
 Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
 Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya washiriki wa 
Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakimsikiliza Waziri 
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa
 LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa 
amesema taarifa ya Kongamano la Uchumi la Dunia la mwaka 2018 inaonesha 
kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na uchumi jumuishi miongoni mwa nchi za
 Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
 Amesema hali hiyo, imetokana na 
Tanzania kufungua fursa za ujasiriamali ambapo kuna zaidi ya biashara 
milioni tatu zinazokuwepo kila mwaka, lengo la nchi ni kuhakikisha kuwa 
uchumi unakua na unamgusa kila Mtanzania hususan mwananchi wa kawaida.
 Waziri Mkuu ameyasena hayo leo 
(Jumatatu, Juni 18, 2018) wakati akifunguaKongamano la Tatu la 
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa 
LAPF, jijini dodoma.
 “Pia, huduma za fedha jumuishi 
ni kigezo ambacho kimeiweka Tanzania mahala pazuri kwenye uchumi 
jumuishi ambapo zaidi ya Watanzania milioni 30 wamekuwa wakifanya 
miamala mbalimbali ya fedha kupitia simu za mkononi na hivyo kuongeza 
huduma za fedha kufikia asilimia 65,” amesema. 
 Amesema huduma za msingi za 
kijamii kama vile elimu, afya na kupungua kwa rushwa katika utoaji 
huduma za umma pamoja namtandao wa miundombinu ya barabara ambayo 
huwezesha wananchi wengi kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ni 
kigezo kingine kilichozingatiwa katika kuipatia Tanzania nafasi hiyo. 
 Waziri Mkuu ameongeza kwamba 
Serikali inaamini kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa 
kasi kubwa na matokeo yake yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, 
soko la huduma na shughuli nyingine za kiuchumi. 
 Katika hatua nyingine, Waziri 
Mkuu amesema suala la uchumi wa viwanda kuelekea uchumi wa kati ifikapo 
mwaka 2025 ni moja ya ajenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo 
amezitaka sekta zote zihakikishe zinatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa
 viwanda.
 Pia amesema suala la uwezeshaji 
wananchi kiuchumi lazima liende sambamba na uwezeshaji vijana kujiajiri 
kama inavyoelekeza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 
2015. “Ilani inatambua kwamba kuwawezesha wananchi kiuchumi ni hatua ya 
msingi katika kujenga Taifa lililoimarika kiuchumi na lenye lengo la 
kujitegemea,”. 
 Aidha, Ilani pia, inasisitiza 
kuhusu umuhimu wa kuhamasisha ushiriki wa Sekta binafsi katika kuwezesha
 wananchi kiuchumi, hivyo ni muhimu kukamilisha taarifa ya uwezeshaji 
kutoka kwa wadau wa sekta binafsi, ili Serikali iweze kuona mchango wa 
sekta binafsi katika kuwawezesha wananchi kiuchumi.
 Waziri Mkuu amesema utekelezaji 
wa malengo hayo ya uwezeshaji wananchi katika maeneo ya fursa za mafunzo
 ya ujasiriamali na mikopo ya masharti nafuu ni muhimu sana katika 
kupambana na umaskini wa kipato. 
Amesema kwa kutambua umuhimu wa 
ajenda ya uchumi wa viwanda, ndiyo maana makongamano ya uwezeshaji 
yamekuwa yakiweka mkazo kwenye masuala ya viwanda. Hali hiyo pia, 
inajidhihirisha katika kaulimbiu ya Kongamano la Tatu ambayo ni: 
“Viwanda: Nguzo ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi”. 
 Hivyo Waziri Mkuu ameongeza kwa 
kusema, “tuendelee kuhimiza kuhusu kutekeleza uchumi wa viwanda kwa 
lengo la kuwawezesha wananchi wetu kiuchumi na kuhakikisha kuwa 
tunafikia lengo la kuwa na  uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,”.
 Kongamano hilo lililoandaliwa na
 Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limehudhuriwa na
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
 Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Kilimo Dkt Charles 
Tizeba, Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage na 
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Bw. Suleiman Jafo.
 Wengine ni Wakuu wa Mikoa 
mbalimbali, Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Dodoma,
 Makatibu Tawala wa Mikoa, Mwenyekiti na Wajumbe wa Baraza la Taifa la 
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,Wakurugenzi wa Halmashauri za Mamlaka za 
Serikali za Mitaa,
Katibu Mtendaji wa Baraza la 
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng’ Issa, wadhamini wa 
Kongamano hilo na Wawakilishi kutoka katika taasisi mbalimbali za 
Serikali na Sekta binafsi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni