Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (Mb), akizungumza wakati wa kikao
cha 52 cha Bunge la 1 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hawa Ghasia
akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu Bajeti ya mwaka wa fedha
2018/19 wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018
Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akijibu swali wakati wa
kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Missungwi
mkoani Mwanza, Mhe. Charles Kitwanga akichangia hoja kuhusu taarifa ya
hali ya uchumi na mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka
2018/19 wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018
Jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiteta jambo na Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Singida, Martha Mlacha wakati wa kikao cha 52
cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Seriikali za Mitaa (OR -TAMISEMI), Mhe. Joseph
Kakunda akijibu swali wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe
18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Phillip Mpango(kulia)na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji wakifuatilia hoja
za wabunge kuhusu taarifa ya hali ya uchumi na mapendekezo ya Bajeti Kuu
ya Serikali kwa mwaka 2018/19 wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11
leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma. (Picha zote na: Frank Shija –
MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………..
Na: Jonas Kamaleki-MAELEZO, Dodoma
Mbunge wa Viti Maalum, Chama cha
Wananchi (CUF), Mhe.Rukia Kassim amepongeza juhudi za Serikali katika
kukuza uchumi ikiwemo kuongezeka kwa pato la Taifa.
Mhe. Rukia ameyasema hayo leo
Bungeni, Jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Serikali kuhusu
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2018/19.
“Naipongeza Serikali kwa hatua za kukuza uchumi hasa ukuaji wa Pato la Taifa unaotarajiwa kuwa asilimia 7.2”, alisema Rukia.
Naye Mbunge wa Urambo, Mhe.
Margreth Sitta ameipongeza Serikali kwa kupendekeza kusamehe Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike.
“Mheshimiwa Spika hatua hii ya
kusamehe kodi hiyo itapunguza bei ya taulo hizo ambayo itawafanya
wanafunzi wa kike kuzipata kwa bei nafuu na kuwawezesha kuhudhuria
masomo kwa muda wote wa masomo ikilinganishwa walivyokuwa wakishindwa
kufanya hivyo wakiwa katika siku zao kwa kukosa taulo”,alisema Mama
Sitta.
Akichangia kwenye bajeti kuu ya
Serikali, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa
anampongeza saa Rais John Pombe Magufuli kwa kujenga miradi mikubwa
miwili ya Standard Gauge naye Umeme wa Stiegler’s Gorge.
“Historia itamwandika Rais
Magufuli kwa kazi kubwa anazofanya hasa kwa ujenzi wa miradi mikubwa
nchini, ule wa reli ya Kisasa (Standard Gauge) na ule umeme wa
Stiegler’s Gorge”, alisema Serukamba.
Aliongezea kuwa bajeti hiyo ni nzuri sana na inapaswa kuungwa mkono kwani inawajali wananchi.
Wabunge wanaendelea kuchangia
bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ambayo iliwasilishwa wiki
iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.
Mwisho
Upinzani Wapongeza Juhudi za Serikali Kukuza Uchumi

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni