Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akielezea ushirikiano walioingia kati benki yao na Kampuni ya Bima ya First Assurance kwa ajili ya kutoa Bima ya Insurance Premium Financing (IPF) kulia ni Bw. Bosco Bugali Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance.
Bw. Bosco Bugali Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance. akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akielezea ushirikiano walioingia na benki ya United Bank For Africa (UBA) kwa ajili ya kutoa Bima ya Insurance Premium Financing (IPF) kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka
Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka akimsikiliza Bw. Dominick Timothy Mkuu wa Kitengo cha Wateja wakubwa (UBA) alipokuwa akielezea jinsi wateja wanavyoweza kupata huduma ya (IPF).
Bw. Bosco Bugali Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka wakipongezana mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari leo.
Bw. Bosco Bugali Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance akimpongeza Loveness Mamuya Meneja Masoko wa First Assuarance mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari leo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
baadhi ya maafisa wa benki ya UBA wakiwa katika mkutano huo.
Bw. Bosco Bugali Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa benki ya (UBA) na kampuni ya bima ya First Assurance mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari leo.
………………………………………………………………………………………………
UNITED Bank for Africa Tanzania(UBA) imetenga Sh.bilioni 23 ambazo zitatumika kukopesha wananchi ambao wanataka kukatia bima mali zao ili ziwe salama.
Hivyo ili kufanikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya kukatiwa bima , UBA wameamua kushirikiana na Kampuni ya Bima ya First Assurance kwa lengo la kuhakikisha wanatoa bima kubwa za aina mbalimbali.
UBA imetenga Sh.bilioni 23 kwa ajili ya kukatia wananchi bima mbalimbali kwa lengo la kulinda usalama wa mali zao.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank for Africa Tanzania Ltd Usman Isiaka amesema lengo la kutoa huduma hiyo ni kuwawezesha wananchi wenye kuhitaji bima kuipata kwa kulipia kwa awamu kwa kipindi cha mwaka mzima.
“Benki yetu itakachokuwa inafanya mteja anapokuja kwetu na kuelezea aina ya bima anayotaka kukata tunalipa fedha yote kwa kampuni ya bima ya First Assurance.
“Baada ya kutoa fedha hizo sisi tutakachofanya ni kumkata mteja fedha awamu kwa awamu kwa kipindi cha mwaka mmoja, ingawa sisi tutakuwa tumelipa yote kwa kampuni ya bima,”amesema.
Amefafanua benki yao pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kibenki imeona haja ya kuwarahisishia wananchi katika kupata bima kwani ni muhimu katika usalama wa mali zao.
Amesema kwa watakaohitaji huduma hiyo hakutakuwa na dhamana ya kuweka mali yoyote zaidi ya kufuata taratibu ambazo wameziweka , hivyo wameomba wananchi kutumia fursa hiyo kwa kupata bima kwa kulipa kidogo kidogo.
Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya First Assurance Bosco Bugali amesema hatua ya benki hiyo kuamua kukopesha wanaohitaji kukata bima itatoa nafasi ya wananchi wengi kupata fursa ya kuwa na bima.
Amefafanua sheria inahitaji anayetaka bima kulipa fedha yote kwa wakati mmoja, hivyo kitendo cha benki ya (UBA) kutoa fedha na kisha mteja kurudisha kwa awamu itarahisisha huduma hiyo.
Ameongeza kuwa kupitia benki hiyo sasa kila mwananchi atakuwa na uwezo wa kukata bima kubwa ambayo faida zake ni nyingi ukkilinganisha na bima ndogo hasa kwenye magari.
Bugali ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima kwa ajili ya usalama wa mali zao na kusisitiza kipindi hiki cha kuelekea Serikali ya viwanda bima ina nafasi kubwa kwani kwa atakayekuwa na kiwanda akikata bima hana wasiwasi na mali zilizopo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni