Hispania imempiga chini, Kocha wake Julen Lopetegui baada ya kuthibitishwa kwamba msimu ujao atainoa Real Madrid.
Kocha huyo alikuwa ajiunge na Madrid kuchukua nafasi ya Zidane baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia linaloanza kesho Alhamisi.
Lopetegui alisaini miaka mitatu na Madrid, lakini wakubwa wa soka la Hispania wamejiridhisha kwamba hawezi kuwa mtu sahihi kuendelea na timu yao kwenye Kombe la Dunia baada ya kupata dili hilo.
Rais wa Chama cha Soka cha Hispania, Luis Rubiales, alirudi Hispania haraka Jumanne jioni akitokea Urussi na kutangaza kwamba Kocha huyo wamemuondoa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni