Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kimataifa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kimataifa. Onyesha machapisho yote

Mama wa kambo 'aamrisha' mwanawe wa kike wa miaka 9 kubakwa na genge la watu



Maafisa wa polisi wamewakamata watu sita kuhusiana na ubakaji wa kikundi na mauaji ya msichana wa miaka tisa nchini India katika jimbo la Kashmir.

Maafisa wanasema kuwa mama wa kambo wa msichana huyo alimwambia mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 14 na wengine watatu kumbaka msichana huyo mbele yake.

Wanasema kuwa mwili wa msichana huyo ulipatikana siku ya Jumapili katika msitu wilayani Baramulla.

Aliteswa na mwili wake kuchomwa na tindi kali , waliongezea.

Mama huyo wa kambo anadaiwa kukasirishwa kwa kuwa msichana huyo alikuwa akipendwa sana na mumewe.

Maafisa wa polisi waliambia BBC Urdu kwamba msichana huyo alitoweka kwa siku kumi kabla ya mwili wake kupatikana.

Ilibainika kwamba mama huyo wa kambo alikuwa na chuki dhidi ya mke wa pili wa mumewe na watoto wake , mtandao wa kituo cha habari cha NDTV kilimnukuu afisa mmoja wa polisi Miir Imtiyaz Hussain akisema.

Bwana Hussein alisema kuwa msichana huyo aliuawa kwa shoka baada ya kubakwa na genge.

Alisema kuwa mmoja ya washukiwa mwenye umri wa miaka 19 alimpiga na kumjeruhi vibaya mwilini.

Hii ni mara ya pili ubakaji mbaya wa aina hiyo umefanyika katika jimbo la Kashmir katika miezi ya hivi karibuni.

Mnamo mwezi Aprili, msichana Muislamu wa miaka minane kutoka Wilaya ya Kathua alibakwa na genge na kuuwawa.

Hatua hiyo ilizua hisia kali baada ya mawaziri wawili kutoka chama cha Hindu Bharatiya BJP kuhudhuria mkutano kuwaunga mkono washukiwa ambao ni Wahindu.

Tatizo la unyanyasji wa kingono nchini India limeongezeka tangu ubakaji wa genge mwaka 2012 na mauaji ya mwanafunzi wa miaka 23 katika basi katika mji mkuu wa Delhi.

Uhalifu huo ulisababisha maandamano ya siku kadhaa na kuilazimu serikali kubuni sheria kali dhidi ya ubakaji ikiwemo hukumu ya kifo.

Hata hivyo mashambulio dhidi ya wanawake na watoto yanaendelea kuripotiwa nchini humo.
Chanzo - BBC

OMAR AL-BASHIR ATEULIWA TENA KUGOMBEA URAIS SUDANI


BASHIR
Rais wa Sudan Omar al- Bashir.
Chama tawala nchini Sudani kimemteua kwa mara nyingine tena Rais wa sasa, Omar al-Bashir kuwa mgombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.
Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba, Bashir aliteuliwa katika mkutano wa chama tawala uliofanyika mjini Khartoum siku ya Alhamisi.
Rais Bashir amekuwa akiiongoza Sudan tangu mwaka 1989 baada ya kuchukua madaraka katika mageuzi ya kijeshi na ameshiriki mara mbili kwenye uchaguzi wa kinyang’anyiro cha urais tangu katiba mpya ya nchi hiyo ilivyopitishwa mwaka 2010.
 Bashir alishinda uchaguzi wa mwaka 2010 na 2015 na amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30, aliwahi kusema siku za nyuma kuwa angeachia madaraka ifikapo mwaka 2020, na alikuwa hajaweka wazi dhamiri yake ya kugombania tena.
Wachambuzi wa kisiasa wanasema kwa kuwa katiba ya Sudan inaruhusu mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja, Bashir ataweza kugombea tu baada ya kubadilisha katiba.
Chanzo: V.O.A Swahili

BAADA YA KUTANGAZWA KUWA KOCHA MPYA WA REAL MADRID,HISPANIA YAMFUTA KAZI YA KUINOA TIMU YA TAIFA


4D273E2700000578-0-image-a-39_1528815805512-634x400
Hispania imempiga chini, Kocha wake Julen Lopetegui baada ya kuthibitishwa kwamba msimu ujao atainoa Real Madrid.
Kocha huyo alikuwa ajiunge na Madrid kuchukua nafasi ya Zidane baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia linaloanza kesho Alhamisi.
Lopetegui alisaini miaka mitatu na Madrid, lakini wakubwa wa soka la Hispania wamejiridhisha kwamba hawezi kuwa mtu sahihi kuendelea na timu yao kwenye Kombe la Dunia baada ya kupata dili hilo.
Rais wa Chama cha Soka cha Hispania, Luis Rubiales, alirudi Hispania haraka Jumanne jioni akitokea Urussi na kutangaza kwamba Kocha huyo wamemuondoa.

MATUKIO KATIKA PICHA HISTORIA ILIVYOANDIKWA TRUMP,KIM JONG UN WALIVYOKUTANA LIVE SINGAPORE


MKUTANO  wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani,  Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini,  Kim Jong Un,  umefanyika nchini Singapore.
Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa Ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili  pekee yao na wakalimani wao.

Mkutano huo ulianza kwa viongozi  hao wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.
Rais Trump amesema wawili hao wamepiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka za makubaliano.

Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama katika rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.
Hata hivyo, haijabainika ni nini kitakuwepo kwenye waraka ambao watautia saini. Trump alisikika akisema kuwa anatarijia makubaliano mazuri katika mkutano huku Kim akisema kuwa haikuwa rahisi kufika hapo.

Mkutano uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu naulifanyika katika Hotel ya Capella katika kisiwa cha utalii cha Sentosa.
Viongozi hawa wakiingia katika mkutano walionekana wenye tabasabu, na kusalimiana kwa kushikana mikono, na baadae Kim Jong Un alimshika bega Trumpa kisha wakaanza kuzungumza kwa msaada wa wakalimani wao.
Baadaye washauri na maofisa mbalimbali walitarajiwa kuingia kuendelea na mkutano huku suala la nyuklia likitarajiwa kujadiliwa kwa kina na haijajulikana bado makubaliano yatakuwa yapi.  Akizungumza kabla ya mkutano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres,  amesema kuwa umoja huo utatoa msaada wowote wa kuhamasisha makubaliano katika mkutano huo.

”Viongozi wawili, wanajaribu kujadiliana jinsi ya kufikia makubaliano ambayo yalileta sana utata mwaka jana, amani na suala la kusitisha nyuklia ndiyo vinabaki kuwa lengo kuu, kama nilivyowaandikia mwezi uliopita kwamba kutahitajika ushirikiano wa hali ya juu na kutakuwa na changamoto za hapa na pale katika makubaliano, Marekani wanatakiwa kusimamia kwa vyovyote hali hiyo,” alisema Guterres.

Mkutano huu unaweza kuwa na mafanikio Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua wawili hao kukutana.
Kwa nini hatua hii imefikiwa hivi sasa?
Mwaka wa kwanza wa Trump katika kiti cha urais ulianza kwa mvutano mkubwa na kurushiana maneno huku Kim naye akiendeleza majaribio ya silaha za nyuklia na kukiuka ilani ya kimataifa. Rais wa Marekani aliapa kupambana ikiwa Pyongyang ingeendelea kuitishia Marekani.

Korea Kaskazini iliendelea kukaidi na kufanya jaribio la nyuklia la sita mwezi Septemba mwaka 2017.
Baadaye Kim alitangaza kuwa nchi yake imefanikiwa katika mpango wake wa kuwa taifa la nyuklia, likiwa na silaha zinazoweza kuifikia Marekani.
Lakini mwanzoni mwa mwaka 2018, Korea Kaskazini ilianza kuboresha mahusiano na Korea Kusini kwa kupeleka timu na ujumbe kwenye michuano ya Olimpiki mjini Pyongyang.
Mwezi Machi, Donald Trump aliushangaza ulimwengu kwa kukubali mwaliko kutoka kwa Kim wa kukutana ana kwa ana.

Tangu wakati huo, njia ya kuelekea mkutano huu ikawa yenye changamoto ambapo Trump alikuwa akiahirisha kila mara kukutana huko.   Lakini hatimaye viongozi hao wamekaa pamoja. Singapore ni nchi ya tatu ambayo Kim Jong-un ameitembelea tangu alipokuwa kiongozi wa nchi yake mwaka 2011.
Safari yake ya kwanza ilikuwa nchini China mwezi Machi na mwezi Aprili akawa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kutembelea Korea Kusini ambapo alikutana na Moon Jae-in.

BALOZI LUVANDA ATEMBELEA WANAFUNZI WATANZANIA WANAOSOMA JIMBO LA PUNJAB NCHINI INDIA


  Hafla hii iliandikwa kwenye magazeti karibu yote ya  Punjab  na kimataifa
 Balozi Luvanda akiwa katika kilemba cha asili akikaribishwa na wenyeji
 Balozi Luvanda akiwa ndugu Yahaya A Mhata  pamoja na  Mr j. S. Bedi chairman na Mkurugenzi Dr Aneet (saree ya njano) wakifurahi na wanafunzi
 Balozi akiwa na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Punjab
 Picha ya pamoja ya wanafunzi na balozi na uongozi wa chuo. Baada ya kucheza basketball. 


 Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania jimbo la Punjab

 Balozi Luvanda akiwa na Bw. Yahaya A Mhata, Bw. J
 

. S. Bedi chairman of Gian jyoti group of institutions 
 
Dr. Aneet(director of Gian jyoti group of institutions) 
Wakisikiliza risala  kutoka kwa wanafunzi wa MBA Bakari Chuma and Irene Boniface
Bw Deepak Singh, akiwasha mshumaa pamoja na ndugu j. S. Bedi chairman Gian jyoti group of institutions wakiwa na Balozi Luvanda




Profesa msaidizi Mrs samarjit Gill akisoma muhtasari kuhusu chuo hicho
 Hafla hii iliandikwa kwenye magazeti karibu yote ya  Punjab  na kimataifa

  Hafla hii iliandikwa kwenye magazeti karibu yote ya  Punjab  na kimat
Mwanafunzi  Bakari Chuma akipiga selfie akiwa na Balozi Luvanda na Mr yahaya Mhata na Mr munish  ambaye ni guide wa rose garden.

 Mwenyekiti  J. S. Bedi na mwanafunzi wa secondary Gian jyoti global schools. Baada ya muheshimiwa kucheza basketball na wanafunzi. Muheshimiwa ni mpenzi wa michezo
  Mkurugenzi wa Chuo Dr Aneet pamoja na wanafunzi wakisubiri kumpokea balozi
 Mwanafunzi Mariam akiwa amevalia vazi linalovaliwa pindi kiongozi ama mtu mashuhuri akiwa anapokewa. 
 Balozi  Baraka luvanda akitoa hotuba kwa wanafunzi na wageni waalikwa
  Balozi Luvanda akiwasha mshumaa kuashiria kuanza kwa hafla hiyo
 Wanafunzi Wakisikiliza hotuba kutoka kwa balozi
Mwambata wa elimu ubalozi wa Tanzania nchini India Bw. Yahya Mhata akipokea shada la maua toka kwa Mwenyeiti wa Gian jyoti groups of institutions Mr J. S. Bedi kushoto
Wanafunzi kutoka mataifa mbali mbali kama Cuba, Mexico, Brazil, Oman, Jamaica, Ghana, Kenya, uganda, Botswana wakisikiliza hotuba ya balozi

 H.E. BARAKA H. LUVANDA (high commissioner, United republic of Tanzania, ndugu Yahaya A Mhata (Education liaison officer, United republic of Tanzania, Mwenyeiti wa Gian jyoti groups of institutions Mr J. S. Bedi kushoto kwa balozi, na Mr Gurdeepak Singh (Dean of international students). And baadhi ya wanafunzi wa kitanzania(mariam Sunday na Vivian Omar) na wengine kutoka mataifa mbalimbali. 
 Muheshimiwa balozi akiwa ndani ya gari yake akiaga baada ya sherehe kumalizika. 
Wanafunzi Mariam, Irene na Vivian wakiwa wamevalia nguo za kipunjab tayari kumpokea muheshimiwa balozi.
 Yahaya A Mhata, ilikuwa ni siku  ya birthday yake na  wanafunzi  wakamuandalia zawadi kidogo. 
 Balozi wa Tanzania nchini India  Mhe. Baraka H Luvanda akiongea na wanafunzi. 
Mwambata wa elimu katika ubalozi wa Tanzania nchini India  Bw. Yahaya Mwinjaka  akiongea na wanafunzi. 

Huenda Cosby akaozea gerezani

Baada ya miongo kadhaa ya minong´ono, uchunguzi na kesi kufuatiliwa kwa karibu, huenda msanii wa Kimarekani  Bill Cosby akaelekea gerezani akiwa na umri wa miaka 80 kwa makosa ya udhalilishaji wa kingono.
Msanii huyo wa vichekesho alipatikana na hatia  siku ya Alhamisi yya kumpa dawa za kulevya na kumdhalilisha kingono mfanyikazi wa Chuo Kikuu cha Temple Andrea Constand katika makazi yake yaliyoko Philadelphia mwezi Januari, 2004.
Wanasheria wanawake  wameutaja uamuzi huo kuwa wa kihistoria. Vuguvugu kwenye mitandao lenye jina #MeToo, limethibitisha kuwa waliokuwa wakimtuhumu Cosby siku zote hawakuwa na makosa: Haiba yake ya uungwana sasa  imevurugwa .
Lili Bernard, aliyesema kuwa Cosby alimdhalilisha kingono kabla ya kumpa nafasi katika kipindi chake maarufu cha "The Cosby Show" mwaka 1992, alijawa na jazba katika mahakama kiasi cha kugonga kichwa chake bila ya kukusudia kwenye meza iliyokuwa mbele yake.
Bill Cosby akiondoka mahakamani Bill Cosby akiondoka mahakamani
"Nimezidiwa na furaha, alisema Bernard nje ya mahakama huku akidondokwa na machozi." Je, nimeamka? Huu ni muujiza."
Zaidi ya wanawake 60 wamelalama kuhusu Cosby
Uamuzi huo, wa kwanza unaomhusisha msanii anayetambulika katika kipindi cha  #MeToo, inahujumu sifa za  msanii mkubwa aliyevuka mipaka ya rangi katika  jukwaa la kuigiza la  Hollywood na kubobea kwenye Televisheni .
Ni moja ya kesi iliotokana na  visa vilivyowakumbuka zaidi ya wanawake 60 waliodai kuwa Cosby aliwapa dawa za kuelevya na kisha kuwadhalilisha kingono kwa kipindi cha miongo mitano, lakini ambao kadhia zao hazikuaminika ama zilipuuzwa kabla ya kuanza kampeni kwenye mitandao ya kijamii yenye anwani #MeToo iliyoangazia dhulma za kingono zilizotekelezwa na wanaume wenye ushawishi mkubwa katika jamii.
Cosby alitumbua macho maelezo ya jaji yakisomwa, lakini baadaye akapaza sauti akimpinga jaji Kevin Steele baada ya mwendesha mashtaka kutaka Cosby apelekwe gerezani mara moja.
Mwendesha mashtaka aliambia mahakama kuwa Cosby ana ndege ya kibinafsi na huenda akiachiliwa akatoroka. Cosby alikanusha kwa hasira kuwa anamiliki ndege na kumtusi mwendesha mashtaka .
Cosby alishtakiwa kwa makosa matatu ya udhalilishaji wa kingono, kila moja likiwa na kifungo cha kati ya miaka mitano hadi 10 gerezani.
Mashtaka hayo huenda yakajumlishwa ama kuunganishwa kwa ajili ya hukumu, lakini ikizingatiwa umri wa Cosby, kifungo chochote kinamaana kuwa huenda akafia gerezani.
Cosby amesema kuwa atakata rufaa
USA Bill Cosby Prozess in Norristown (picture-alliance/newscom/J. Angelillo) Bill Cosby anakabiliwa na makosa matatu ya udhalilishaji wa kingono
Utekelezaji wa kifungo chake huenda ukafanyika katika kipindi cha miezi mitatu. Kabla ya hayo Cosby lazima afanyiwe uchunguzi kuthibitisha iwapo kuwa ni mtumiaji wa nguvu wa dhulma za kingono. Aidha atajiandikisha kuwa mkosaji wa kingono kwa kuzingatia sheria za Megan.
Jopo la wanaume saba na wanawake watano lilishauriana kwa muda wa masaa 14 kabla ya kutoa uamuzi dhidi ya Cosby.
Constand- 45, mfanyikazi wa Chuo Kikuu cha Temple, alisema Cosby alimlemaza kwa kumpa tembe tatu kisha akakosa fahamu, kisha akamdhalilisha kingono kwa kutumia vidole vyake alipokuwa amelala hana nguvu za kukubali ama kukataa. Cosby anadai kuwa kitendo hicho kiliafikiwa na wote.
Cosby aliupungia mkono umati ambao ulikuwa nje ya mahakama na kuingia kwenye gari lake na kuondoka bila ya kusema chochote. Wakili wake Tom Mesereau alitangaza, "vita havijakamilika" na kusema kuwa atakata rufaa.
Mawakili wa upande Cosby wakiongozwa na Mesereau, aliyeshinda kesi dhidi ya Michael Jackson kuhusu kuwadhalilisha watoto kingono, walishambulia Constand wakati wa kesi hiyo huku wakimuita muongo ambaye alimsingizia Cosby kwa lengo la kutaka kuwa tajiri.

LIVERPOOL YAIZAMISHA TENA MANCHESTER CITY UEFA


Timu ya Liverpool imetinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu kupita miaka 10 baada ya kutokea nyuma kufungwa goli moja na kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manchester City.

Wenyeji Manchester City walianza vizuri kwa kumiliki mpira tangu mwanzo wakijaribu kubadili matokeo ya mchezo uliopita ya kufungwa magoli 3-0 na alikuwa Gabriel Jesus aliyefunga goli la kwanza.

Liverpool ilichomoa goli hilo katika kipindi cha pili kupitia kwa Mohamed Salah mnamo dakika ya 56, kufuatia pasi ya kutanguliziwa na Sadio Mane kisha baadaye zikiwa zimesalia dakika 13 Roberto Firmino akaongeza la pili.
                 Mohamed Salah akifunga goli la kusawazisha lililochangia kubadilisha mchezo

   Kocha Jurgen Klopp akipiga ngumi hewa kushangilia goli alilofunga Mohamed Salah

Balozi Wilbroad Slaa Awasilisha Hati Zake Za Utambulisho Kwa Mfalme Wa Sweden


SeeBait
Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Wilbroad Slaa jana akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden.

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Wilbroad Slaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa ofisi ya Mfalme wa    Carl XVI Gustaf wa Sweden baada ya utambulisho