Rais Shein awataka Wafanyakazi wa Wakala wa matukio ya Kijamii Zanzibar kutoa huduma zinazostahiki kwa Wananchi


DSC_3146
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Muhammed Shein  akizungumza na wananchi  na Wafanyakazi wa Wakala wa Usaji wa Matukio ya Kijamii Zanzibar baada ya Uzinduzi huo (kuli) Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Haji Omar Kheir na  Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt. Hussein Khamis .
DSC_2839
Wafanyakazi wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ( hayupo pichani) baada ya Uzinduzi wa Ofisi yao  katika Kijiji cha Dunga Mkoa wa Kusini Unguja.
DSC_2851
Wananchi wa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ( hayupo pichani) baada ya Uzinduzi wa Ofisi ya  Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar .
Na Maryam Kidiko / Fatma Makame – Maelezo.              4/9/2018.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraa la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amewataka Wafanyakazi wa Wakala wa matukio ya Kijamii Zanzibar kutoa huduma zinazostahiki kwa Wananchi ili kupata taarifa sahihi katika kazi zao.
Hayo aliyasema huko Dunga Mkoa wa kusini Unguja wakati akizindua Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukiuo ya Kijamii Zanzibar.
Alisema ili kupata taarifa sahihi na kujua idadi ya watu lazima kujenga masharikiano makubwa baina yao  na Wananchi.
Alisitiza Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inahitaji takwimu sahihi hivyo Wafanyakazi nilazima kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria, kanuni na uadilifu.
Aidha aliwataka wafanyakazi hao kuelimisha jamii juu ya suala zima la kujisajili katika matukio ya kijamii na kupambana na changamoto zitazojitokeza ili ziweze kuleta maendeleo.
“Katika kazi hii changamoto mbali mbali zitajitokeza hivyo ni muhimu kupambana na changamoto hizo kwa kuzifanya ziweze kuleta mafanikio” alisema Rais Shein.
Hata hivyo Rais wa Zanzibar alitoa wito kwa wananchi na wageni  kutumia vizuri fursa hiyo na kila mmoja awe tayari kutoa taarifa sahihi zinazomuhusu.
Amewaomba Wafanyakazi wanaohusika na usajili wa matukio ya kijaamii Zanzibar kuwa majukumu yao yanagusa sehemu mbali mbali hivyo waandae mikakati sahihi na taarifa ili waweze kufanikisha malengo waliyokusudia.
Akielezea zaidi alisema kuwa ili kupatikana maendele na kuimarisha Sekta mbali mbali ni muhimu kushirikiana na kuendeleza jukumu la kulinda amani iliopo katika Nchi.
Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa  na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir alisema kuwa sheria iliyowekwa inataka matukio yote ya kijamii ni lazima yasajiliwe .
Alisema kuwa kila kitu kimekamilika na tayari kuanza rasmin kwa kufanya usajili kwa Wakaazi wa Zanzibar pamoja na wageni waliokuwepo Zanzibar.
Alilisisitiza kuwa upo umuhimu mkubwa kwa wageni kwa upande wao kusajiliwa kwani wanasehemu yao tofauti na wenyeji wa Zanzibar.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni