YALIYOJIRI BUNGENI LEO SEPTEMBA 4, 2018


1 (2)
Mbunge wa Jimbo la Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza akiapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job NdugaiS leo Jijini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
2 (2)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimpongeza mbunge wa Buyungu Mhe. Mhandisi Christopher Chiza mara baada ya kula kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job  Ndugai leo Bungeni Jijini Dodoma.
5
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.  Dkt. Mary Mwanjelwa akieleza mikakati ya Serikali katika kuinua sekta ya kilimo hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
4 (2)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani   Jafo akiwasilisha Bungeni maelezo ya Serikali kuhusu muswaada wa sheria ya kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wa mwaka 2018( The Dodoma Capital City ( Declaration) Bill, 2018.
3 (2)
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali Bungeni Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwezesha mikoa kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo ili kuinua uchumi wa mikoa hiyo.
8
Mbunge wa Kibakwe Mhe. George Simbachawene akisisitiza kuhusu faida za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi yetu leo Bungeni  Jijini Dodoma.
6 (1)
Sehemu ya wabunge wakifuatilia  mkutano wa  12 kikao cha kwanza cha Bunge leo Jijini Dodoma.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni