WANAHABARI WATAKA RAIS MAGUFULI AKOMESHE WATU WANAOSABABISHA MANYANYASO KWA WAANDISHI


Jopo la majaji wa Tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2018 limemtangaza Mwandishi wa habari I wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2018.
 
 
Tuzo hiyo imetangazwa leo Jumanne Septemba 4,2018 wakati wa mkutano mkuu wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania UTPC unaofanyika katika ukumbi wa Lush Garden Hotel jijini Arusha.
Kushoto ni Absalom Kibanda Mhariri mkuu kutoka gazeti la. Mtanzania akikabidhi tuzo ya Daudi Mwangosi 2018 kwa mke wa Azory Gwanda.Katikati ni rais wa UTPC,Deogratius Nsokolo
Kushoto ni Absalom Kibanda akikabidhi cheti cha utambuzi kwa mke wa Azory Gwanda
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, Ndimara Tegambwage akitangaza mshindi wa tuzo ya Mwangosi 2018.
 
Mbali na kukabidhiwa tuzo hiyo,pia amekabidhiwa cheti cha utambuzi pamoja na shilingi milioni 10.
Jopo la Majaji wa Tuzo ya Mwangosi Mwaka 2018, wakwanza kulia ni mwenyekiti wa jopo hiloNdimara Tegambwage, Katikati ni mama Edda Sanga, na wengine wawili. 
 
Na Vero Ignatus. Arusha

Mwanahabari Mkongwe nchini Absolom Kibanda  ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania amemuomba Raisi Magufuli achukue hatua juu ya matukio ya kupotea  kwa Wanahabari akiwemo  Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi ambaye alipotea miezi 9 iliyopita katika mazingira ya kutatanisha.
 
Kibanda amesema kwa Rais Magufuli amekua akisifia juhudi za Wanahabari hivyo asiishie  katika kusifia bali achukue hatua ili kuponya majeraha ya Wanahabari ambao wanakamatwa na kuteswa huku wengine wakipotea kwenye mazingira ya utata
 
Absolom Kibanda amevitaka vyombo vya dola kubaini alipo Azorry Gwanda ambaye ametoweka kwenye mazingira ya kutatanisha kwa takribani miezi 9 sasa na hajulikani alipo.
 
Kibanda ambaye ni Mgeni rasmi aliyekabidhi Tuzo ya Daudi Mwangosi kwa Mke wa Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Azory  ambaye amepotea kwa takribani miezi tisa katika mazingira ya kutatanisha.
 
Aidha ameitaka Wizara husika kuchukua hatua na kufanya uchunguzi na kubaini ili Azory aweze kupatikana na kuendelea na majukumu yake ya Kitasnia.

“Vyombo vya dola vikate mzizi wa fitina kwa kuwakamata wanaohusika na vitendo vya kikatili kwa wanahabari ikiwemo Kupotea kwa Azory ,kuteswa kwa Kibanda ,kumwagiwa tindi kali Kubenea” Alisema Kibanda
 
Amesema katika mitandao kuna Taarifa 17500 Zinazoelezea tukio la Azory  kwenye mitandao ya kijamii  hivyo suala hilo bado linagonga vichwa katika vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa.
 
Mke wa Azory ,Anna Pinuni  amepokea tuzo hiyo huku akigubikwa na machozi ,pia ameshukuru kwa tuzo hiyo na kuishukuru kampuni ya Mwananchi kwa kumjali na kumtunza tangu siku ya kwanza mume alipopotea.
 
Anna ambaye kwa sasa ana mtoto mchanga wa miezi 6 ,mume wake alipopotea alikua na ujauzito wa miezi 6 .
 
Raisi wa Muungano wa Vilabu vya Wanahabari nchini UTPC Deudatus Nsokolo  amesema kuwa vyombo vya habari vinapaswa uwajali wanahabari hasa wanapoingia katika matatizo pia kuiga mfano wa Kampuni ya Mwananchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni