WAJASILIAMALI WATAKIWA KUJENGA UCHUMI WA TANZANIA

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF, Bathow Mmuni wakati akifunga mfunzo ya Sido yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka wajasiliamali kuendelea kuwa wabunifu kwa kutenegeza bidhaa zenye ubora.

"Nawaomba wajasiliamali mtengeneze bidhaa zenye ubora na nzuri zitakazowavutia wateja ili mtakapoziuza zitachangia pato la taifa kukua zaidi," alisema Mmuni. Aliongeza kuwa kwa sasa NSSF wamejipanga kurudi kuanza kuwasaidia wajasiliamali ili kukuza kipato chao ili waweze kuendeleza uchumi wa viwanda. 


Kwa upande wa Mkurugenzi wa Sido- Dar es Salaam, MacDonald Maganga aliwaomba wajasiliamali wote walipo mtaani kuchangamkia mafunzo ya Sido ili yaweze kuwaongezea ujuzi na kuzifanya bidhaa zao zikawa na thamani zaidi.

"Wajasiliamali jitokezeni kokote pale mlipo mchangamkie mafunzo tunayoyatoa maana yamekuwa yakiwajenga zaidi kwa kuongeza ubora wa bidhaa mnazozitengeneza, ukiangalia katika kundi lenu hili kuwa watu wameshaanza kutengeneza bidhaa ila wamekuja kujiongezea ujuzi zaidi jambo ambao ni jema zaidi maana unapopata cheti cha Sido kitakusaidia kuweza kupenya katika soko," alisema Maganga.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mfunzo ya wajasiliamali yaliyoendeshwa na Sido mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akiwa ameshika chaki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeshwa nguo ya batiki iliyotengenezwa na wajasiliamali waliokuwa waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bathow Mmuni akionyeswa mafuta na sabuni walizotengeneza wajasiliamali waliopata mafunzo ya Sido-Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi wa Sido Dar es Salaam, MacDonald Maganga.
Mjasiliamali Suleiman Nassoro Mohamed ambaye ni Katibu wa BAKWATA akisoma risala wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo.
Baadhi ya wajasiliamali wakipatiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo.
                                               Wajasiliamali wakiwa katika picha ya pamoja.

AFRIKA YAAZIMIA KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Aliyasema hayo jana (Jumatatu Januari 29, 2018) alipozungumza baada ya mkutano wa Viongozi wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika Mkutano huo ambao Waziri Mkuu alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, alisema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.

Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

Alisema nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia amapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme.

“Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umene na sasa inamikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita.

Alisema miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ya tume iliyokuwa inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.

“Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC.”

Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.

Alisema Tanzania ilihusika kutoa mchango juu suala la amani na usalama katika nchi za Afrika. ambapo kila nchi inawajibika kujilinda yenyewe na kulinda nchi jirani pamoja na Jumuia zake.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 30, 2018.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz, nje ya ukumbi wa Nelson Mandela mjini Addis Ababa, Waziri Mkuu yupo Nchini Ethiopia, kumwakilisha Rais John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika AU. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, wakati alipo mtembelea kwenye Hoteli ya Radisson Blue, mjini Addis Ababa Ethiopia. Januari 30, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DK. KIGWANGALLA AWATAKA WALIOVAMIA KIWANJA CHA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO KILICHOPO NJIRO, JIJINI ARUSHA KUJIANDAA KISAIKOLOJIA


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipata maelezo ya eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82 ndani ya eneo hilo kutoka Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi (katikati). Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jinala Bodi ya Utalii Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82. Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jinala Bodi ya Utalii Tanzania.
Meneja wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Egidius Mweyunge (kulia) akimuongoza Waziri Kigwangalla kukagua eneo hilo.
Dk. Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua eneo hilo.

MPINA AAGIZA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA VICTORIA KUANZA KAZI IFIKAPO JULAI MWAKA HUU


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Bi Anarozy Nyamubi kuteketeza nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni katika wilaya ya Musoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emanueli Bulayi akishuhudia tukio hilo leo.(Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anarozy Nyamubi baada ya kuteketeza nyavu haramu katika Wilaya ya Butiama leo. (Na John Mapepele)
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akimwaga mafuta kwenye nyavu haramu ili kuzichoma moto katika kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo. (Na John Mapepele)

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo ambapo alishiriki zoezi la kuchoma nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi cha kudhibiti uvuvi haramu Kanda ya Ziwa Victoria alichokiunda hivi karibuni, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent Anney akisoma majina ya Wavuvi Haramu (Na John Mapepele)

Asisitiza operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ziwa ni ya kudumu

Na John Mapepele, Mara

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata samaki na mazao yake vilivyofungwa katika Mikoa ya Mwanza na Mara kuanza kazi mara moja ifikapo Julai Mosi mwaka huu, ambapo amewataka wamiliki kupeleka mipango kazi ya namna ya kuvifufua kabla ya kufikia mwezi Machi mwaka wizarani kwake.

Alivitaja viwanda hivyo kuwa ni Tan Perch Limited na Supreme Perch Limited vilivyopo Mwanza na Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited katika mkoa wa Mara.

Waziri Mpina alizungumza hayo jana wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara na Mwanza kukagua operesheni maalum ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ya Ziwa Victoria inayofanywa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni.

“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Uvuvi nchini niliyepa kulinda raslimali za uvuvi nitahakikisha kwamba ulinzi wa raslimali hizi ni wa kudumu, na usio na mwisho hadi uvuvi haramu utakapoisha hapa nchini” alisisitiza Mpina

Waziri Mpina alipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa huo, wananchi katika maeneo tofauti na hatimaye kushiriki katika zoezi la kuchoma nyavu haramu ambapo hadi sasa zaidi ya nyavu zenye thamani ya shilingi bilioni nne zimechomwa moto katika zoezi linaloendelea la kudhibiti uvuvi haramu mkoani Mara.

Kamanda anayeongoza kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara, Bakari Lulela alimweleza Waziri Mpina kuwa operesheni hiyo imefanyika katika Wilaya za Musoma, Butiama, Rorya na Bunda na kufanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu zenye thamani ya sh. bilioni 3.2 huku wavuvi na wafanyabiashara wa samaki na mazao yake waliokiuka sheria ya uvuvi wakitozwa faini ya sh. milioni 189.

Waziri Mpina aliziagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua Maafisa Uvuvi wa Kijiji cha Bwai Kumsoma waliotuhumiwa kushirikiana na wavuvi haramu kuondolewa mara moja katika kijiji hicho ili kupisha uchunguzi na ikithibitika wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vincent Anney amesema kwamba hayuko tayari kuona Wilaya yake inaendelea kuishi na watumishi wanaojihusisha na uvuvi haramu na kwamba sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika wilaya hiyo.

Aidha Waziri Mpina ameiagiza Wizara yake kuandaa bei elekezi ya kununua samaki itakayowezesha kuondokana na tabia ya wenye viwanda kushusha hovyo bei pindi samaki wanapoongezeka na hivyo kuwadhulumu wavuvi kupata malipo stahili yanayotokana na kazi yao.

Waziri Mpina alisema Ziwa Victoria ni hazina na raslimali kubwa kwa Tanzania ambapo inaaminika kuwa ni la kwanza kwa ukubwa katika bara la Afrika kwa kuwa na eneo la 68,000Km2 na la pili duniani.

Alisema pamoja na umuhimu wa ziwa hili katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania bado linakabiliwa na shughuli za uvuvi haramu uliokithiri ambapo tafiti zinaonyesha kwamba kama hakutakuwa na jitihada za haraka za kutokomeza uvuvi haramu, ziwa hilo hali halitakuwa na raslimali za uvuvi ikiwa ni pamoja na samaki katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Alitaja uvuvi haramu unaofanywa kuwa ni pamoja na kuvua katika maeneo yasiyoruhusiwa, kutumia valiyombo visivyosajiliwa, kuvua bila leseni,kutumia sumu, kutumia nyavu za utali na kuvua samaki wachanga ama wazazi wasioruhusiwa.

Uvuvi haramu mwingini nikuvua kwa kokoro na nyavu zenye macho madogo chini ya kiwango kinachokubalika kisheria, katuli, kumbakumba na gizagiza ambapo alisema Serikali imedhamilia kutokomeza uvuvi huo haramu.

Aidha alisema operesheni hiyo katika kanda ya Ziwa Victoria dhidi ya uvuvi haramu ni ya kudumu na inafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi Na.22 yaMwaka 2003 na Kanuni 58(1) ya Uvuvi ya Mwaka 2009 na Sheria ya Mazingira Na 20 ya Mwaka 2004 kifungu Na(1), 65(1)a pia Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Na 29 ya Mwaka 1994 ili kudhibiti uvuvi haramu ulioshamiri kiasi cha kutoweka kwa raslimali ya samaki katika ziwa hilo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Waziri Mpina alisema Tanzania inamiliki 51% ya Ziwa hili ikifuatiwa na Uganda 43% na nchi ya Kenya inamiliki 6%. Ziwa hili ni moja ya maziwa yanayozalisha samaki kwa wingi duniani kwa makadirio ya takribani tani 1,000,000 kwa mwaka ambapo asilimia 60 ya uzalishaji wa samaki wake unatoka Tanzania hivyo juhudi za pamoja za kutokomeza uvuvi haramu zinahitajika

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MTEULE DKT. WILBROD SLAA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuzungumza na wanahabaari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS DK. SHEIN AFUNGUA WARSHA YA UELEWA JUU YA MAMLAKA YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO ZANZIBAR ( SMID )


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kulifungua Kongamano la Warsha ya Uelewa Juu ya Mamlaka Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogona Vya Kati (SMIDA) hafla hiyo imewashirikisha Wajasiriamali mbalimbali wa Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi kikwajuni Zanzibar.(Pcha na Ikulu)
KATIBU Mkuu Wizara ya Viwanda na Masoko Zanzibar Juma Ali Juma akizungumza kitaalamu juu ya Uelewa Juu ya Mamlaka ya Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogo Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Tanzania Profesa Sylvester M Mpanduji, akitowa maelezo juu ya umuhimu wa uaznzishaji wa Viwanda Vidogo vidogo kwa wajasiriamali wakatikwa warsha hiyo ilioandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar iliofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi Kikwajuni.
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali, akitowa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kulifungua Kongamano hilo.

BAADHI ya Wajasiliamali wa Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo wakati wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifufunga Warsha hiyo ililofanyika katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi kikwajuni Zanzibar.

BAADHI ya wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua Kongamano la Warsha la Kutoa Uelewa Juu ya Mamlaka Itakayosimamia Viwanda Vidogo vidogo na vya Kati (SMIDA) lililoandaliwa na Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa katika picha ya pamoja na Watoa Mada wa Warsha Hiyo baada ya kufunguliwa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, na kulia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali wenye viwanda Zanzibar .
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, na kulia Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali.Picha na Ikulu)

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAAFISA WAKUU WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WANAOTARAJIWA KUSTAAFU.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael Isamuhyo watatu kutoka
(kulia) Brigedia Jenerali Aron Robert Lukyaa wapili kutoka (kulia),
Kanali Peter Samuel Sameji wa kwanza (kulia). 


 Wengine katika picha ni Brigedia Jenerali William Ephraim Kivuyo wapili kutoka kushoto na Brigedia Jenerali Elizaphani Lutende Marembo. PICHA NA IKULU

MAWAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WA TANZANIA NA RWANDA WAJADILI UJENZI WA RELI YA ISAKA- KIGALI

Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano kuhusu upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (kushoto) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Eugene Kayihura (kulia) wakiwa katika majadiliano ya pamoja kabla ya kuanza kwa mkutano kuhusu namna ya kupata fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.
Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) ukiendelea kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (kulia) wakiondoka baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na kutoka Rwanda ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakisaini maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakibadilishana taarifa walizosaini za maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)