Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametishia kung’oa kiongozi mkubwa wa Chadema ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
Ameyasema hayo mara baada ya madiwani wawili wa CHADEMA kuachia ngazi Mjini Iringa, ambapo amesema kuwa hoja za madiwani hao wanakimbia ubabe wa mchungaji Msigwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo.
"Leo Madiwani wengine wawili wamehama na kujiunga na CCM. Ukiwasikiliza kilichowaondoa ni Uongozi Mbovu na Ubabe pale Iringa Mjini. Nasikia wameambiwa "never outshine your master". Mimi nilidhani "masta" ni wananchi kumbe ni "pasta". Ukitukana tusi moja Kiongozi mmoja nachomoa DSM " Ameandika Polepole
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la viongozi wa kisiasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kuhamia chama tawala cha CCM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni