Mkazi wa maili 35 amuomba waziri wa afya msaada aokoe maisha ya mwanae

 Bi Flora Liberia (33) akiwa yupo na mwanae Samweli Amos miaka (2)akiwa nyimbani kwakwe Maili 35 kata ya Visiga Halmashauri ya mji wa Kibaha mkoa wa Pwani.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus Pwani.

MKAAZI wa eneo la Maili 35  Kata ya Visiga  katika Halmashauri ya Kibaha Mjini Bi Flora Liberia (30) ameelezea masikitiko yake kutokana na kutaabika na ulezi wa mtoto wake Amos Samwel mwenye umri  wa miakamiwili na nusu ambaye tangu alipozaliwa viungo vyake havijakaza hali iliyosaabisha kukumbana na muuguzi aliyedai kuwa ni mfanyakazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  ambaye amekuwa akimlaghai na kutumia fedha zake kwa madai kuwa atamsaidia kumpatia matibabu mtoto huyo.

Ameongeza kwa kusema  yeye hana ajira hivyo hulima vibarua vunavyomwezesha kupata ujira  mdogo ambao hujichangisha  ili aweze kumpatia matibabu  mtoto wake ambaye tangu alipomzaa  viungo vyake havijawahi kuwa imara kama ilivyo kwa watoto wengine anazungumza hayo  kwa masikitiko .

Bi Flora ameomba  msaada kutoka kwa Waziri mwenye dhamana Mheshimiwa Ummy Mwalimu ili kuweza kuokoa maisha ya mtoto wake.

Mtoto Samweli Amos miaka( 2) alizaliwa 2015 1/3 Zahanati ya mlandizi iliyopo Kibaha mkoa wa Pwani,aliwa ameketishwa katika kiti walichotengeneza wazazi kwaajili ya kumketisha mtoto huyo kama inavyoonekana hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.

 Wa kwanza kushoto ni baba mzazi wa mtoto samweli ,Amos Hussein (39 mwenyeji wa Morogorokatikati ni Samwel Amos (2) wa kwanza kulia ni mama yake  Flora Liberia (33 )mwenyeji wa Kigoma,ila kwa sasa wanaishi mtaa mail 35 kata ya Visiga Halmashauri ya mji wa  Kibaha mkoa wa Pwani.Picha na Vero Ignatus Blog.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni