WAZIRI DKT MABULA ATAKA UWAJIBAKI KWA MAKAMISHNA WA ARDHI KUFIKIA MALENGO YA WIZARA

Na Ahmed Mamoud Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka Makamishna Wasaidizi wa Ardhi wa mikoa nchini kuwajibika na kutumia wajibu wao katika kutekeleza mikakati ya Wizara kufikia malengo. Aidha, amewataka Makamishna hao kuwapangia majukumu kwa malengo maafisa walio chini yao na kufuatilia kazi wanazowapa mara kwa mara. Dkt Mabula amesema, hayo tarehe 25 Februari 2022 wakati akifungua kikao kazi cha Menejiment na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi wa mikoa kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha. ‘’Yapo malamiko ya lugha zisizofaa kwa wateja, hii haikubaliki fuatilieni hili na kulikemea vikali na kuzingatia misingi na kanuni za utumishi wa umma katika majukumu yenu ya kila siku ’’ alisema Dkt Mabula. Aidha, aliwataka katika utekelezaji mpango mkakati wa wizara wanazingatia vipaumbele vya serikali hususan maelekezo ya mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kupitia kodi ya pango la ardhi. Akigeukia suala la makusanyo ya kodi ya pango la ardhi, Waziri wa Ardhi aliwataka Makamishna wa ardhi Wasaidizi wa mikoa kuwa wabunifu katika njia za kukusanya mapato. ‘’Sula la mtandao kutopataikana muda mwingi linaonekana kuwa kikwazo katika ukusanyaji maduhuli, lifanyieni kazi’’ alisema Dkt Mabula. Waziri Dkt Mabula pia alihimiza kuongezwa kwa kasi ya umilikishaji ardhi na kuwataka Makamishna hao na wakuu wa idara katika wizara kuweka malengo kwa kila ofisa mwenye taaluma ya ardhi kuandaa hati. Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi alisema baada ya kuteuliwa alifanya ziara katika baadhi ya mikoa na kukutana na baadhi ya changamoto alizozitaja kuwa ni pamoja na kutofikiwa malengo ya ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na baadhi ya halmashauri kutohudumia idara za ardhi kwa madai ya idara hizo kuhamishiwa wizarani. ‘’Nimeanza kuchukua hatua ili kutatua changamoto hizo ambapo tayari nimetoa maagizo mbalimbali kwenye mikoa na menejimenti ya wizara na ni matarajio kikao kazi kutaibua suluhisho la changamoto hizo’’ alisema Dkt Allan Kijazi. Kwa mujibu wa Dkt Kijazi, Wizara ya Ardhi imekuwa ikinyooshewa vidole na wananchi kwa masuala ya ukiukwaji wa haki za wananchi na kuchafua taswira ya Wizara na kutaka watendaji wa sekta ya ardhi kujitafakari na kujisahihisha kwa kutimiza wajibu ili kuondoa dhana hiyo. Aligusia pia mpango wa urasimishaji makazi holela na kueleza kuwa, ni matarajio yake kupitia kikoa hicho washirikia wataibuka na mkakati wa uelekeo wa wizara katika kupanga miji sambamba na usimamamia fedha zilizotolewa kwa ajili ya mpango wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi maarufu kama KKK.

MASHINDANO SED MISS VALENTINE'S 2022 KUFANYIKA KESHO

Mashindano ya Sed Miss Valentine's 2022 yatafanyika kesho februari 14 mwaka 2022 Mjini Babati Mkoani Manyara huku warembo 15 wanatarajiwa kuchuana vikali kutwaa taji hilo. Afisa Masoko wa Kiwanda cha Mati Super Brand Gwandumi Mpoma ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wakazi wa Babati wanafurahia mashindano hiyo amewataka wajitokeze kwa wingi. Gwandumi amesema kuwa Mashindano hayo yanalenga kuibua vipaji vya vijana na kuwapa fursa ya kufanya kazi na kiwanda hicho kupitia bidhaa mbali mbali wanazozalisha ikiwemo Strong Gin,Sed Pinepale na Tanzanite Premium Vodka. Hamisi Saidi ni Moja kati ya waandaaji wa Mashindano ya Sed Miss Valentine amesema kuwa warembo wamejiandaa vizuri katika kambi hiyo na wanatarajia ushindani utakua mkali kutokana na maandalizi waliyoyafanya. wa Upande wao washiriki wa Mashindano hayo Jenifer Paulo Mmari na Keithwin Pallangyo wamepongeza udhamini wa kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kuwawezesha kukaa kambini na kujiandaa vyema hivyo wamewataka wakazi Mkoa wa Manyara na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi.