Mashindano ya Sed Miss Valentine's 2022 yatafanyika kesho februari 14 mwaka 2022
Mjini Babati Mkoani Manyara huku warembo 15 wanatarajiwa kuchuana vikali kutwaa
taji hilo. Afisa Masoko wa Kiwanda cha Mati Super Brand Gwandumi Mpoma ambao
ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha
wakazi wa Babati wanafurahia mashindano hiyo amewataka wajitokeze kwa wingi.
Gwandumi amesema kuwa Mashindano hayo yanalenga kuibua vipaji vya vijana na
kuwapa fursa ya kufanya kazi na kiwanda hicho kupitia bidhaa mbali mbali
wanazozalisha ikiwemo Strong Gin,Sed Pinepale na Tanzanite Premium Vodka. Hamisi
Saidi ni Moja kati ya waandaaji wa Mashindano ya Sed Miss Valentine amesema kuwa
warembo wamejiandaa vizuri katika kambi hiyo na wanatarajia ushindani utakua
mkali kutokana na maandalizi waliyoyafanya. wa Upande wao washiriki wa
Mashindano hayo Jenifer Paulo Mmari na Keithwin Pallangyo wamepongeza udhamini
wa kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa kuwawezesha kukaa kambini na
kujiandaa vyema hivyo wamewataka wakazi Mkoa wa Manyara na Mikoa jirani
kujitokeza kwa wingi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni