MABALOZI WA USALAMA BARABARANI ARUSHA WAMSHANGAZA KAMANDA MPINGA


 Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. PICHA NA GADIOLA EMANUEL
  Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akikagua "Birthday Surprise Cake " aliyopewa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akipokea Chupa ya Shampeni kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bw. Bakari Msangi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akigonga Cheers na  Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga wakishiriki shampeni na Mabaozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Daniel Urioh akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga huku kulia akishuhudiwa na Mwenyekiti. Bi. Stella na Kushoto ni Balozi Wilbard Ngambeki katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.

 Balozi Mustafa Panju akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Wilbard Ngambeki akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Seria Tumainiel akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Vero Ignatus akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Balozi Vero Ignatus akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga huku mwenye kiti akishuhudia katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akikata "Birthday Surprise Cake " huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Balozi Mustafa Panju akimlisha keki Kamanda Mpinga kwa niaba ya wazee waliopo katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha
   Kamanda Mpinga akimlisha Keki Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha
 Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani akimlisha keki Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha
 Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani wakipongezana na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha
 Kamanda Mohamed Mpinga akifurahia mlo wa usiku na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha
 Kamanda Mohamed Mpinga akipata mlo wa usiku na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha
 
 Kamanda Mohamed Mpinga akipata picha ya pamoja na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha



Mabalozi  wakizungumza na kufurahi ujio wa Kamanda Mpinga Jijini Arusha na kututafuta Mabalozi katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha,  Picha Zote na Gadiola Emanuel.




 Mabalozi wa usalama wa barabarani (Road Safety Ambassadors - Arusha) wamesherehekea sikukuu ya
kuzaliwa ya Kamanda Mohammed  Mpinga jijini Arusha.

Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Milestone Park -Sakina ,
imeandaliwa na kamati ya (RSA -Arusha) chini ya mwenyekiti wa mkoa Bi. Stella
Rutaguza na kuhudhuriwa na wajumbe wa( RSA - Arusha)

"Kwakweli mmenistua jamani sikutegemea kama mmeniandalia jambo kubwa
kama hili ,nilijua nakuja kukutana tu na mabalozi ili kufahamiana na
kuongelea maswala yetu ya usalama barabarani "alisema Mpinga.

DCP Mpinga mbaye yupo kikazi jijini Arusha alikutana na mabalozi wa
usalama barabarani,kwa lengo la kuongelea na kujadili  maswala ya usalama
barabarani na mabalozi hao,ambao kazi yao kubwa ni kuelimisha
jamii,kukemea na kuripoti matukio yanayoathiri usalama barabarani,na
kushawishi mabadiliko ya tabia ,sheria na sera.

Amezungumzia changamoto iliyopo kwa sasa kwa utoaji wa risiti pale
dereva anapotakiwa kulipa faini kutokana na makosa yanayofanyika
barabarani,amesema kuwa mfumo huo wa kieletroniki tayari umeshaanza
kutumika jijini Dar-es-salaam na hivi karibuni mfumo huo utaanza
kutumika katika mikoa sita iliyopewa kipaumbela kabla ya mwaka huu
kumalizika.



Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Arusha,Pwani,Morogoro,Mbeya,
Dodoma,
na Mwanza,na amewataka askari wa usalama barabarani kutumia lugha
njema kuwaelewesha madereva pale wanapohitaji kupewa risiti za(
EFD)ili waweze kutambua changamoto hiyo kwa sasa ambayo serikali
inalishughulikia.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Bushbuck safaris Bw. Mustafa Panju amemuomba
mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha SSP. Eng.Nuru
Suleimani ampe ruhusa ya kutoa mafunzo kwa askari wa usalama barabarani
Arusha kuhusu huduma kwa mteja.


"Nipo tayari kutoa ofa ya mafunzo kwa askari wetu wa kikosi cha usalama
barabarani ukinipatia nafasi ,na hii itasidia sana " Alisema Panju.


 Naye mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Bi.  Stella
Rutaguza amempongeza Kamanda Mpinga katika siku yake ya kuzaliwa na
kumtakia maisha marefu, yenye afya tele.



Bi. Stella ameongeza kuwa katika mkoa wa Arusha kutakuwa na oparasheni
Abiria paza sauti itakayofanyika kwa miezi mitatu lengo kuu likiwa ni
kumjengea uwezo na kumuhamasisha dereva na abiria kuchukua tahadhari
kuepuka ajali.

Amesema kampeni hii inalenga kumfanya abiria atambue haki na wajibu
wake ,akiwa kwenye basi APAZE SAUTI pale panapotokea uendeshaji
hatarishi barabarani,na pia kumfanya dereva abadili mtazamo wake na
kujenga utamaduni wa usalama barabarani,hii inamfanya dereva na abiria
kuwa sehemu ya suluhisho la ajali za barabarani.

KIGWANGALA:WANAWAKE WANAOFANYA NGONO BILA KINGA WANAUWEZEKANO MKUBWA WA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI




Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala akiwa anazungumza na waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi, katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini Arusha.,aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mountmeru iliyopo jijini Arusha.

 Waandishi wa habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala,Aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital
Waandishi wa habari wanawake wakifuatilia kwa karibu baadhi ya majibu ya yaliyokuwa yakijibiwa na madaktari walioendesha mafunzo,mafunzo hayo yalikwenda sambaba na upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi.

Na Mahmoud Ahmad Arusha.
 

Naibu waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV vinavyosababisha   Saratani ya mlango wa kizazi
 
Kigwangala amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa  kwa kujaamiana .

Kigwangala amesema  kuwa kati ya wanawake 100,000 wanawake 50.9% wanaweza kupata saratani ya Shingo ya kizazi,na kati ya hao asilimia 37.5% wanapoteza maisha hivyo serikali imeanza kutekeleza utafiti wa mradi ambao utahusisha wasichana wenye umri kati ya miaka 9-14 katika wilaya ya Moshi na utakapokamilika wataanza utoaji wa chanjo hiyo kwa nchi nzima,amewataka kutokufanya ngono mapema.

Amesema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi haionyeshi dalili wala maumivu yeyote amesema mgonjwa anaweza akawa nao kuanzia miaka 10-15 bila kujitambua huku dalili zikiwa zinakwenda taratibu sana.

Kwa upande wake Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya mount Meru amesema kuwa dalili za Sratani ya Mlango kizazi ni kutokwa na damu bila mpangilio,kutokwa na majimaji yenye harufu kali,amewataka wanawake watakapoziona dalili hizo wawahi hospitali mapema kabla tatizo halijawa kubwa.

Aidha Masumuni amesema kuwa unaweza kujikinga ili usipate saratani ya mlango wa kizazi kwa kupima saratani ya mlango wa kizazi mapema,kupunguza idadi ya kuzaa watoto wengi,kupunguza idadi ya wpenzi wengi,ukifanya ngono watumie kinga.

Sambamba na hayo Dkt.Mwanahamisi Lyinga amesema kuwa zipo njia kuu tatu za kupima saratani ya mlango wa kizazi mabazo ni pamoja na kutumia Darubini,Upimaji wa( DNA)wa kirusi,pamoja na Via utambuzi wa kuona kwa kutumia Siki.

Kwa upande wake Sr.Noela Lyinga ambaye ni muuguzi katika hospitali ya Mountmeru ametoa elimu kwa wanawake wawe wanajikagua matiti yao kila wanapomaliza mzunguko wao wa hedhi kila mara ili kuona kama yapo mabadiliko katika matiti yao ambayo yanaweza kuleta saratani ya matiti.

Lyinga amewataka wanawake mara wanapoona dalili yeyote  ambayo siyo ya kawaida katika matiti yao wasisite wawahi hospitali mapema wakafanyiwe uchunguzi na vipimo ili kama utagundulika ugonjwa waweze kupatiwa matibabu kwa haraka zaidi. .

WADAU WAJADILIANA JINSI SEKTA BINAFSI INAVYOWEZA KUSHIRIKI KATIKA MKAKATI WA UTEKELEZAJI THABITI WA MPANGO WA PILI WA MIAKA MITANO WA MAENDELEO YA TANZANIA, (FYDPII)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, (kulia), akizungumza kwenye Warsha ya majadiliano ya wadau kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano (FYDPII), kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mkoawa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka
Naibu Katibu Mkuu Tume ya Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy(kushoto0, akizungumza kwenye warsha hiyo.

                                      Baadhi yawashiriki wa warsha wakifuatilia mjadala
                                                         Baadhi ya washiriki

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka, akizungumza wakati wa warsha hiyo

NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

WADAU kutoka kada mbalimbali wamekutana kujadiliana jinsi sekta binafsi itakavyoshiriki katika utekelezaji thabiti wa mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, amesema sekta binafsi inao umuhimu mkubwa katika kushiriki kuandaaa na kujadili mipango mbalimbali ya maendeleo.

Dkt. Kida aliyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Warsha ya majadiliano kuhusu nafasi ya sekta binafsi katika kutekeleza mpango wa pili wa miaka mitano wa maendeleo ya Tanzania, (FYDP II) iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na ESRF, Serikali kupitia Tume ya Mipango na Mpango wa Kusaidia Mabadiliko ya Kiuchumi, (SET), iliwakutanisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, (TPSF), CEO roundtable, Suma JKT, Taasisi ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) , wadau wa maendeleo kutoka Jumuiya ya Ulaya, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na wasomi.

Dkt. Kida alisema, Majadiliano hayo nimatokeo ya juhudi zilizoanza tangu 1998-200, ambapo ESRF ilishiriki katika uanzishwaji wa mpango wa Taifa wa Vision 2025 uliolenga kuitoa Tanzania kwenye kundi la nchi masikini hadi zile zenye uchumi wa Kati, (Middle income coutry.

“Mwaka 2011 ESRF ilifanya mkakati wa kupitia mpango huo wa vision 2015 na kubaini masuala kadhaa ambayo yalihitaji kuelezewa kama kweli taifa linaelewa mpango huo wa kipindi kirefu.” Alisema na kuongeza ni hivi karibuni sisi katika ESRF tulifanya mapitio ya mkakatiwa kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDPI), na MKUKUTA II, mapitio ambayo yamechangia kuingia katika Mpango huu wa pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, (FYDP II), Alisema Mkurugenzi huyo Mtendaji wa ESRF.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Tume ya Mipango, kutoka Wiraza ya Fedha na Mipango, Dkt. Maduka Paul Kessy alisema, “Kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia katika mkakati huu ambayo wajumbe mtalazimika kuyafanyia kazi kwa kina ambayo ni pamoja na kutambua kwamba nchi yetu imedhamiria kuingia kwenye uchumi wa viwanda, kwa hivyo rasilimali tulizonazo tuhakikishe zinalisha viwanda vyetu mfano tunapaswa tujadiliane ni kwa namna gani tunafikia hatua ya kuchakata pamba na ngozi hapa hapa nchini, na utengenezaji wa madawa.”, aliwaambia washiriki wa warsha hiyo.

Ili kutekeleza hilo, Viongozi wa Wilaya na Mikoa hawana budi kushirikiana na sekta binafsina kujadili namna ya kutekeleza maswala haya ili kusudi ifikapo mwishoni mwa Novemba mwaka huu, tutakapokutana tujue nini kilicho mbele yetu, alifafanuaDkt. Kessy.

Akitoa mada yake kuhusu ushirikishwaji wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka alisema, “Wakati umefika sasa, watanzania kuanzisha viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya mazao na mifugo ili kuboresha maisha na kuondokana na tatizo la vijana kukosa kazi.

Akitolea mfano, Mkuu huyo wa mkoa ambaye ameteuliwa na Rais John PombeMagufuli kuogoza mkoa huo akitokea wilayani Mvomero mkoani Morogoro, alisema. “Sisi Simiyu tumepiga hatua, hivi sasa tunatengeneza chaki sisi wenyewe kwa matumizi ya shule, na tunataka pamba tunayolima ambapo Simiyu ndio mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa zao hilo, tuanze kutengeneza vifaa vya hospitalini vinavyotokana na zao la pamba. “ Alifafanua Mkuu huyo wa Mkoa kijana.

Bw. Mtaka pia alisema, asilimia 50 ya mifugo inatoka mkoani Simiyu na moja ya mkakati alioufanya kuwashirikisha SIDO na wadau wengine katika kuanzisha kiwanda kidogo cha kuongeza thamani ya maziwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa na nia yetu ni kusambaza viwanda vya aina hii kwenye kila wilayani 
Mkurugenzi wa Mpango wa kusaidia mabadiliko ya kiuchumi, (SET), Dkt.Dirk Willem te Velde, akizungumza kwenye warsha hiyo
Mtafiti Mkuu wa Taasisi ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii, (ESRF), Profesa Samwel Wangwe, akitoa mada kuhusu masuala ya utekelezaji wa mpango huo na mapungufu, kutokana na funzo la mipango iliyopita
Katibu Mtendaji wa CEO-Roundtable, Bi. Santona Benson, akifungua warsha hiyo kwa niaba ya  Taasisi hiyo, Bw. Ali Mufuruki. 
                             Mjumbe akipitia machapisho wakati wa warsha hiyo

                                  Maafisa kutoka SUMA-JKT nao walikuwepo
Katibu Mtendaji wa CEO-Roundtable, Bi. Santona Benson(kushoto), akifafanua baadhi ya mambo. Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Bw. Anthony Mtaka, na Mkurugenzi wa ESRF, Dkt. Tausi Mbaga Kida
                     Dkt. Kida, akipeana mikono na Mkuu wa Mkoa, Bw. Anthony Mtaka
        Dkt.Dirk akitoa mada juu ya misingi ya utekelezaji thabiti     ya              mikakati ya utekelezaji wa mpango huo


                            Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha hiyo
                                                                    Picha ya pamoja

DC MUHEZA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA ZAHANATI MPYA YA KIJIJI CHA ZENETI

 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi,Mwanasha Tumbo katika akiongozwa na Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Mwenyekiti wa Serikali ya  Kijiji cha Zeneti wakitembelea Jengo jipya la Zanahati ya Zeneti iliyojengwa kwa ushirikiana baina ya Halmashauri,Wananchi na Shirika la World Vision na Mbunge wa Jimbo hilo ambalo limegharimu kiasi cha milioni 35.2
 Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akimuongozwa Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyetembelea zahanati ya Zeneti kuona jinsi inayoendelea na ujenzi wake kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti
 Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiingia kwenye vyumba vya zahanati mpya ya Zeneti kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Lwiza Mlelwa



 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akisisitiza jambo kwa Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi

 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiangalia baadhi ya vyoo vya Zahanati hiyo wakati alipoitembelea kuikagua na kuona namna ujenzi wake unavyoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akiwaonyesha kitu diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza,Mathew Mganga kulia wakati alipoitembelea Zahanati ya Zeneti
Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi akizungumza na wananchi  katika ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya katika Zahanati ya Kijiji cha Zeneti
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Zeneti akiongea kwenye ziara hiyo ya mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zeneti wakati za ziara ya Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Zeneti Kata ya Potwe wilayani humo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akipitia taarifa ya ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Zeneti iliyopo Kata ya Potwe wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa nne kutoka kushoto akiwasilikiza wananchi waliokuwa wakiulioza maswali kwenye ziara hiyo
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Zenethi Kata ya Potwe wilaya ni Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye alifanya ziara ya kutembelea ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akisikiliza kero ya mmoja wa wananchi ambaye alimfuata mara baada ya kumalizika mkutano baina yake na wananchi hao kulia ni Diwani wa Kata ya Potwe,Rashid Mdachi
 Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mikakati waliojiwekea kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi changamoto za Afya.