Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo
ameshiriki ujenzi wa daraja fupi(drift) katika kijiji cha Orgirah kata ya
Mundarara na tarafa ya Engarenaibow kwa lengo lakuhamasisha wananchi na
viongozi wengine.
Akitoa msisitizo kwa viongozi kujitoa sana pale
wanapoitajika kushiriki shughuli mbalimbali za
maendeleo kwa wananchi wao hasa zile ambazo zimeanzishwa kwa nguvu za
wananchi wenyewe.
“Viongozi mbalimbali wasiwe wazito kujitoa
katika shughuli kama hizi za maendeleo ya wananchi na hasa ambazo zimeanzishwa
kwa nguvu za wananchi wenyewe nivema basi na serikali nayo kupitia viongozi kwa
ngazi tofauti kujitokeza nakuunga mkono”.
Mradi huo wa daraja fupi(drift) ulianza rasmi
mnamo Octoba ,2016 kwa lengo lakuunganisha vijiji viwili vya Orgirah na
Igulailungwa ambavyo vilitenganishwa kwa ukosefu wa daraja hilo fupi na
kupelekea kwa vijiji hivyo kukosa mawasiliano.
Aidha mradi huo mpaka kukamilika utagharimu
kiasi cha shilingi milioni 9 ambapo mpaka sasa ni milioni 6 tu ndio zimetumika
katika ujenzi huo, ikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido ilichangia 450,000,
Mkurugenzi wa halmashauri alichangia 640,000 na nguvu za wananchi ni milioni 5.
Hata hivyo Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa
juhudi walizozianza za ujenzi huo na hivyo serikali itawasaidia pale penye
mapungufu na wananchi wenyewe wanatakiwa kujitokeza zaidi hususani kwenye
shughuli kama hizo za maendeleo.
Mradi huo bado unamapungufu ya shilingi milioni
2 ili kukamilisha milioni 9 kama gharama nzima ya ujenzi na Mkuu wa Mkoa
aliaidi kuchangia mifuko 30 ya simenti,pesa taslimu 500,00 na kutoa katapila
ikiwa wananchi watakuwa tayari kuchangia mafuta.
Meneja wa TANROAD Arusha
Enginia John Kalupale aliaidi kuchangia mifuko 50 ya simenti.
Pia mwenyekiti wa chama cha CCM Mkoa Lekule Ole
Laiza atachangia mifuko 30 ya simenti, mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido bwana Sabore Molleiment
atachangia 500, 000, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Juma Muhina nae atachangia
400,000 na Halmashauri yenyewe itaenda kujadili kwenye vikao vyake namna
yakusaidia ujenzi huo.
Gambo bado yupo ziarani Longido huku
akishirikiana na wananchi wa Wilaya hio katika shughuli mbalimbali za maendeleo
yao.
Wananchi wa kijiji cha Orgirah wakishiriki katika ujenzu wa daraja fupi(drift) kwenye kijiji chao. |
Hili ndilo daraja fupi(drift) lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Orgirah kata ya Mundarara Wilayani Longido. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni