WAHUDUMU WATAKIWA KUJIENDELEZA KIELIMU

  1. Mkurugenzi wa kituo cha Rrograss Centre Rose Urio akishirikiana na Veta akiendesha mafunzo kwa wahuduma wa mahoteli mbali mbali ya jiji la Arusha ambapo muitikio wake umekuwa chini na kuonyesha kuwa bado wananchi wanaishi kwa mazoea kwenye kazi zao picha na mahmoud Ahmad Arusha
  2.  
  3. Baadhi ya wahudumu wa hotel mbali mbali za jiji la Arusha walioshiriki semina ya siku mbili ya uboreshaji wa huduma za kuwahudumia wageni mbali mbali katika kuboresha suala zima la utalii na wageni mbali mbali wanaofiki kwenye hotel zao
  4.  

  5.  
  6. Wadau mbali mbali walioshiriki kutoa mada wakiandaa mada katika semina hiyo
  7.  
  8.                                                           washiriki wakifuatilia makini
  9.                                                                      Mafunzo yakiendelea
  10.                                                     Baadhi wakiwa makini kufuatilia mafunzo
  11. WANAHABARI HAWAKUWA NYUMA KUFUATILIA MATUKIO HAYO
  12.  
  13.       
  14. Mafunzo yakiendelea kwa wahudumu hao wa mahoteli mbali mbali




  15. TAASISI ya kusaidia kuinua ubora wa huduma za Hotel nchini, Prograss centre ya jijini Dar es salaam, imeamua kuendesha mafunzo kwa wahudumu wa hotel za jijini Arusha ili waweze kutoa huduma bora kwa wateja na kuvutia wageni na kulinda ajira zao .
  16. Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Rose urio, amesema mafunzo hayo yenye lengo la kuboresha huduma kwenye hotel yanatolewa kwa kushirikiana na VETA yanalenga kuwawezesha wamiliki na wahudumu wa hotel nchini kuwa na uwezo mkubwa wa kuhuduma za Hotel na kuvutia wateja.
  17. Amesema mafunzo hayo ambayo yataendeshwa nchini kote kwa awamu yanatolewa kutokana na kuwepo kwa upungufu wa uelewa kutoka kwa baadhi ya wamiliki na wahudumu ya namna ya kuhudumia wateja kwa viwango vyenye ubora vinavyotakiwa  .
  18. Urio, amesema Veta na taasisi yake  zinatambua ushindani mkubwa uliopo kwa wahudumu wa hotel wa ndani na  nje ambapo hotel nyingi zimeaajiri wahudumu kutoka nje kutokana na uhodari na weledi wao kuwa ni mkubwa ukilinganisha na wahudumu wazawa.
  19. .Amesema kinachokwamisha upatikanaji wa huduma bora ni kutokana na wamiliki wa hotel kuajiri ndugu au watu wenye uhusiano wa karibu ambao hawana uelewa mkubwa wa soko la ushindani katika nchi za jumuia ya afrika mashariki na matokeo yake ni kushuka kwa biashara kwenye hotel zao.
  20. Urio ,amesema kutokana na hali hiyo ya kutokuwa na mbinu za viwango vya juu vya kibiashara, taasisi hiyo ya Progress Centre, kwa kushirikiana na VETA, imeona njia pekee ya kuwaimarisha wahudumu wa hotel za hapa nchini ni kuwapatia mafunzo na  hivyo kuwawezesha kuhimili ushindani kutoka kwa wahudumu wan je ambao wanatishia ajira zao.
  21. Urio, amesema kuwa mafunzo hayo pia yatashirikisha mama lishe na wamiliki wa migahawa ili waache kufanya shughuli kwa mazoea bali waboreshe huduma kulingana na ushindani uliopo na kuondoa malalamiko ya wazawa kukosa ajira .
  22. Amesema mafunzo hayo yanatolewa kutokana na kubaini kuwepo upungufu kwa baadhi ya wahudumu na wamiliki wa Hotel, ambao wamekuwa wakishindwa kuhimili ushindani katika soko la jumuia ya Afrika mashariki na matokeo yake ni kuajiriwa wahudumu wa hotel kutoka nje kwa kuwa wana viwango na uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja . 
                                        



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni