WAALIMU WASTAAFU NAO HAWAKUWA NYUMA KAMA HAPA WAKIFUTILIA MKUTANO HUO.Picha zote na mahmoud ahmad arusha
MKUU wa wilaya ya Arusha, Gabriel Fabian Daqarro, amemugiza
afisa Usitawi wa jamii wa halmashauri ya jiji la Arusha kuhakikisha wazee wote wa jiji hilo
wanapatiwa vitambulisho kabla ya mwisho wa mwaka huu ili waweze kupata huduma mbalimbali
ikiwemo matibabu kwenye Hospitalini mbalimbali.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano na
wazee wa jiji la Arusha uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa
,AICC, ulikuwa una lengo la kusikiliza kero za wazee ili zipatiwe ufumbuzi pia
kufahamiana.
Mkuu huyo wa wilaya ameiagiza Idara hiyo kuhakikisha
vitambulisho vinapatikana kabla ya mwisho wa mwezi, sanjari na kuwataka
watendaji wa serikali, mashirika ya umma na taasisi mbali mbali za serikali
katika jiji la Arusha kuhakikisha kuwa zinatoa kipaumbele kwa wazee ambao
wamekuwa hawapati huduma zao kwa wakati.
Aidha amewataka wenyeviti wa mitaa,kata na tarafa
kushirikiana na jeshi la na jeshi la
polisi kuhakikisha wanaimarisha usalama kwenye maeneo yao ili kuwezesha wazee
kuishi kwa usalama bila kubughudhiwa na kuhakikisha wanasiamia maadili.
‘’Mumepewa madaraka ya kuimarisha ulinzi yatumieni ili wazee
wasibughudhiwe ,tambueni kuwa wazee ni muhimu ndio waliotufikisha hapa sasa
sitaki kusikia kuwa wanasumbuliwa sitaki kusikia malalamiko ya ya kuporomoka
kwa maadili ””alisema Daqarrro.Wakichangia
kwenye mkutano huo wazee wamedai kuwa taasisi za fedha pamoja na
halmashauri ya jiji haziko tayari kuwakopesha wazee kwa hofu ya kuwa watakufa
karibuni na kutaka dhana hiyo iondoke
kwa kuwa kuzeeka sio kufa .
Wamesema nao wana mahitaji mbalimbali ya kuendesha sghuhuli
zao za kiuchumi hivyo wanayo haki ya kupewa mikopo kama yalivyo makundi mengine
ya jamii.
Wameomba kushirikishwa kuanzia ngazi ya mtaa hadi
halmashauri ili wawe na wawakilishi wao ambao watawasilisdha kero zao kwenye
vikao vya maamuzi vya serikali na baraza la madiwani pia wapate uwakilishi
bungeni kama yalivyo makundi mengine ya walemavu, vijana na wanawake.
Wamelalamikia kukosa Vitambulisho ambavyo vingeliwawezesha
kupata huduma za haraka kwenye taasisi mbalimbali za serikali,ikiwemo dawa
kwenye hospital za serikali, pia wamelalamikia lugha za kuwadharirisha
zinazotolewa na baadhi ya wahudumu wa hospital za serikali na vituo vya afya.Wamelalamikia
hatua ya Zahanati kutokutoa huduma siku za mwisho wa wiki hali ambayo
inawasababisha kukosa huduma za matibabu.Aidha wamelalamikia TASAF kutoa fedha
kwa ajili ya watu wasiokuwa na uwezo kwa upendeleo ambapo walengwa wamekuwa
hawanufaiki na mpango huo wa TASAF.
\ |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni