DC Kasesela akiteta jambo na naibu meya wa Manispaa ya Iringa Bw Lyata
Na Matukiodaima BLOG
SERIKALI
wilayani Iringa imepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na
kituo cha msaada wa kisheria cha LASWA mkoani Iringa na kutaka
kituo hicho kuendelea kupeleka vijijini wasaidizi wa kisheria ili
kuwasaidia wananchi kujua haki zao na kuagiza wananchi
kuwafichua matapeli wanaokopesha wananchi mikopo ya riba kubwa .
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa warsha ya ufunguzi wa mradi wa kuimarisha
huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa
haki kwa wananchi wote hasa kina mama wajawazito iliyotolewa kwa
madiwani wa wilaya nzima ya Iringa na watendaji wa kata jana katika
ukumbi wa chuo kikuu huria cha Tanzania , mkuu wa wilaya ya Iringa
Richard Kasesela alisema kuwa kumekuwepo na utapeli unaofanywa na
baadhi ya watu kupitia mikopo hiyo kwa kuwatoza wananchi riba kubwa
jambo ambalo halitavumiliwa .
Kwani
alisema kuwa kumkopesha mwananchi mkopo si kosa ila pale
inapotokea mkopeshaji kumtaka mwananchi huyo kulipa riba mara mbili
ama tano ya mkopo aliokopa ni sawa na utapeli hivyo wananchi
wasisite kuwafichua wale wote wanaofanya utapeli wa aina hiyo .
"
Nawaagiza wale wote wanaofanya utapeli wa kukopesha wananchi
mikopo ya riba kubwa kuacha mara moja vinginevyo nitawashughulikia
kwa kuwachukulia hatua kali ......haiwezekani wananchi kuendelea
kuumizwa na mikopo hiyo na baadhi yao kupokonywa nyumba zao kwa
kushindwa kulipa riba kubwa wanazodaiwa "
Mkuu
huyo wa wilaya alitaka LASWA kupitia wasaidizi wake wa
kisheria mijini na vijijini kuendelea kuwasaidia wananchi ambao
wananyanyasika kwa kutojua sheria pamoja na kutetea wale wote
wanaokandamizwa na matapeli hao wa mikopo hiyo ya riba kubwa .
Kuhusu
watendaji wa serikalini na baadhi ya mahakini wa mahakama za
mwanzo zilizopo vijijini wanaotumika kuwakandamiza wananchi
wasiojua sheria mkuu huyo alitaka kila diwani kufikisha taarifa
ofisini kwake ili mahakimu hao na watendaji wanaopindisha sheria
kwa kujinufaisha kuchukulia hatua za kinidhamu .
Alisema
kuna baadhi ya mahakimu vijijini wanatumika kunyanyasa wananchi
kwa kupindisha sheria kusudi ili kujipatia fedha .
"Kuna
hakimu mmoja sitaki kumtaja jina ila yupo Halmashauri ya Iringa
vijijini kwa kusudi anatumika kutoa hukumu kandamizi na kwa
kushirikiana na mteja wake anashinikiza aliyeshinda kesi kufungua
kesi ya madai ili fedha hizo wagawane......huu ni unyanyasaji mkubwa
kwa kumpokonya haki mwenye haki ili kumpa asiye na haki"
Hivyo
alisema mafunzo hayo kwa madiwani na watendaji hao wa kata ni
vema yakatumika kuwakomboa wananchi kwa kuwasaidia kujua sheria na
kuwafichua wale wanaokiuka sheria na kuomba LASWA kuweka vijana
wao waliopewa mafunzo ya kisheria kila ofisi ya mkuu wa wilaya ili
kusaidia mambo ya kisheria badala ya kuwategemea wanasheria wa
Halmashauri .
Mkurugenzi
wa LASWA Francis Mwilafi alisema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na
asasi yake ya LASWA kwa ufadhili wa LSF ya jijini Dar es salaam
kwa chini ya ubalozi wa Denmark kuwa sifa ya msaidizi wa
kisheria ni kuwa na akili timamu pia sifa ya kuheshimu na kulinda
sheria za mbali mbali za nchi na haki za binadamu
Mkurugenzi
huyo alisema hadi sasa wamekwisha toa mafunzo na kuwa na vijana
katika wilaya zote tatu za mkoa wa Iringa ikiwemo ya Kilolo,
Mufindi na Iringa kwa kuwa na vijana wasaidizi wa kisheria
Aidha
alisema faida kubwa ya msaidizi wa kisheria ni kupunguza na kuziba
pengo la ukosefu wa huduma za msaada wa kisheria katika jamii
anayoishi kwa kutoa usaidizi wa awali wa kisheria. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni