Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki
 yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi
 ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga 
Veterinary Dar es Salaam.
 Mwonekano wa pikipiki hiyo kwa nyuma.
Pikipiki hiyo ikiwa katika kijiwe hicho cha  Veterinary Maganga Temeke jijini Dar es Salaam.
Na Dotto Mwaibale
PIKIPIKI yenye namba za usajili T 684 
CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika kituo 
cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Temeke jijini Dar es 
Salaam inazua hofu kwa wananchi na hata kwa askari polisi ambao 
wameshindwa kuipeleka kituoni.
Imeelezwa kwamba pikipiki hiyo 
iliegeshwa katika eneo hilo na mtu mmoja ambaye alifika nayo akiwa 
akiiendesha mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza jana na mtandao wa www. habari za jamii.com mmoja
 wa waendesha bodaboda wa kituo hicho ambaye hakupenda kujitambulisha 
jina lake alisema pikipiki hiyo inawapa hofu wananchi wa eneo hilo na 
hata waendesha bodaboda.
"Hata sisi wenyewe tuna hofu na pikipiki
 hii ndio maana tunaegesha mbalimbali na pikipiki zetu na ndio maana 
sitaki kutaja jina langu" alisema mwendesha bodaboda huyo.
Aliongeza kuwa awali baada ya pikipiki 
hiyo kutelekezwa katika kituo hicho mtu yeyote alipokuwa akiisogelea au 
kuigusa ilikuwa ikijiwasha yenyewe lakini baada ya kupita mwezi mmoja 
iliacha kujiwasha jambo ambalo limeongeza hofu kwa wananchi.
Mkazi mwingine wa eneo hilo 
aliyejitambulisha kwa jina moja la Ismail alisema hata walipotoa taarifa
 kituo cha polisi cha Maganga walishindwa kuichukua pikipiki hiyo 
kutokana na tabia ya kujiwasha.
Alisema aaskari wa kituo hicho ambacho 
kipo mita 10 na eneo ambalo ipo pikipiki hiyo walitoa taarifa kwa wenzao
 wa kituo cha Chang'ombe ambao nao wameshindwa kuichukua na kwenda nayo 
kituoni kwa ajili ya kumtambua mmiliki wa pikipiki hiyo kupitia namba 
zake za usajili.
Ismail alisema inawezekana pikipiki hiyo
 ilifungwa kifaa maalumu cha utambuzi iwapo kama imeibiwa na ndio maana 
ilipokuwa ikiguswa au kusogelewa inajiwasha yenyewe licha ya baadhi ya 
watu wanahusisha kujiwasha kwake na imani za ushirikina.
Imeelezwa kuwa pikipiki hiyo wakati 
inatelekezwa ilikuwa katika hali ya upya lakini hivi sasa imeanza 
kupoteza upya wake kwa kukosa huduma ya matunzo.
Jitihada za mtandao huu kumpata 
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo wa Maganga ili kuzungumzia suala hilo
 zimeshindika baada ya kuelekezwa alikuwa Manispaa ya Temeke kwenye 
mkutano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni