Mkuu
 wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, 
Ernest Makale, akitoa taarifa ya kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister
 Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ 
na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata 
nafasi ya kujiunga na jeshi hilo kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Na BMG
Makale
 ameeleza kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kujipatia kiasi cha 
shilingi 240,000 kati ya shilingi 500,000 alizokuwa ameomba kutoka kwa 
mmoja wa walioomba kujiunga na JWTZ.
Amebainisha
 kwamba mtuhumiwa mmoja ambaye ni mstaafu wa JWTZ aitwaye Sophia Chacha 
amekuwa akimsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa 
wakihitaji kujiunga na jeshi ambapo ili kupata nafasi hiyo mtuhumiwa 
amekuwa akihitaji kiasi cha shilingi 500,000.
Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 10 mwaka huu katika hoteli moja iliyopo Kirumba Jijini Mwanza kufuatia mtego wa maofisa wa TAKUKURU.
"Kitendo
 cha mtuhumiwa kujifanya afisa wa jeshi hakihusiani na makosa yaliyo 
chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namaba 11/2007, hivyo 
jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa 
wakili wa serikali mfawidhi ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani 
kujibu tuhuma zinazomkabili". Alifafanua Makale.
Aidha
 Makale ameongeza kwamba TAKUKURU wilayani Misungwi imemfikisha 
mahakamani Katibu wa Idara ya Utumishi wa Waalimu TSD wilayani humo kwa 
kosa la tuhuma za kupokea rushwa shilingi 400,000 kutoka kwa Kitoki 
Mgaya ili asimchukulie hatua za kinidhamu kazini.
Mkuu
 wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, 
Ernest Makale, akitoa taarifa ya kwa wanahabari kuhusu kukamatwa kwa 
mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari 
wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini 
Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ kupitia maofisa 
anaofahamiana nao.
Mtuhumiwa
 Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la 
Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili 
awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ.
Kushoto
 ni mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa 
Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini 
Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ. Kulia ni Sophia
 Chacha ambaye ni mstaafu wa JWTZ anayetuhumiwa kumsaidia mtuhumiwa huyo
 kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na JWTZ.
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni