BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA YATAKIWA KUTENGENEZA FURSA ZITAKAZOSAIDIA UPATIKANAJI WA FEDHA KWA HALMASHAURI NCHINI.



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano wa  kuzindua Bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa leo mjini Dodoma. 
Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia elimu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Bw. Benard Makali akizungumza katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma. 
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa wakifuatilia uzinduzi wa Bodi hiyo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa leo mjini Dodoma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene akikata utepe wa nyaraka muhimu zinazohusu Bodi, katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene kwenye picha ya pamoja na wajumbe  wa bodi ya mikopo na baadhi ya watumishi wa bodi hiyo katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.

Na, Nasra Mwangamilo

Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa yatakiwa kuongeza fursa itakayoziwezesha Serikali za Mitaa nchini kupata fedha za kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene alipokuwa akizindua rasmi Bodi hiyo leo mjini Dodoma.

“Natambua kuwa nyenzo muhimu za kutekeleza majukumu ya Bodi ni rasilimali fedha ambazo zinatakiwa zipatikane kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo vimeainishwa kwa mujibu wa sheria, kifungu cha 62 cha Sheria ya Bodi ya mikopo kinataja njia mbalimbali ikiwemo kupata fedha kama zitavyoainishwa na Bunge kwa madhumuni ya kuendesha shughuli za Bodi”.Aalisema Mh. Simbachawene.

Aidha alisisitiza kuwa Bodi hiyo ijitahidi kusimamia kwa ukaribu zaidi uwekezaji kwa kuelekeza rasilimali kwenye vitega uchumi vyenye faida kubwa ikiwa ni njia mojawapo ya kujiongezea mapato huku ikiwa na lengo la kuhakikisha inatoa mikopo kulingana na makubaliano baina ya Bodi na Halmashauri husika.

Pia aliwataka wa jumbe wa Bodi kusimamia kwa ukaribu utendaji wa Bodi hiyo na kuhakikisha kwamba hesabu zinatunzwa vizuri na taarifa zinatolewa kwa wakati hii ni pamoja na kuweka amana za muda maaalumu kwenye mabenki, umiliki wa hisa katika mabenki, kodi ya pango kutoka kwenye nyumba zinazomilikiwa na Bodi pamoja na malipo ya riba kutoka kwenye mikopo.

“Nitumie nafasi hii kusisitiza kwamba nanyi kama wa jumbe wa bodi hii lazima kusimamia kwa ukaribu utendaji wa bodi ya mikopo na kuhakikisha kwamba hesabu zinatunzwa vizuri, Ni vizuri taarifa za bodi zipatikane kwa wakati nakuwasilishwa mbele ya bodi na kujadiliwa kwa wakati”. Alisisitiza Waziri.

Kukosekana kwa mwamko wa kimaendeleo miongoni mwa baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri hivyo kuna umuhimu wa bodi hii mpya kusaidia kuchochea ubunifu wa kimaendeleo ili Halmashauri ziinue miradi bora inayokopesheka na yenye faida kubwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni