Mkuu
 wa mkoa wa Kilimanjaro,Said mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa
 msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi 
Msamadi ,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya 
kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.  
 Mkuu
 wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki kuchimba msingi kwa ajili
 ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo 
wilayani Hai.  
 Kaimu
 Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Juliet Mushi akishiriki kuchimba msingi 
kwa ajili ya ujenzo wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi 
iliyopo wilayani Hai.  
 Baadhi
 ya wananchi wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi 
wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi.  
 Msingi
 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya 
msingi Msamadi ukiwa umechimbwa na wananchi wakati wa uzinduzi wa 
kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule zilizoko 
wilaya ya Hai.  
 Mkuu
 wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza wakati akizindua 
rasmi kampeni za kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya 
ya Hai.  
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.  
 Mkuu
 wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi juu ya wazo 
la kuanzishwa kwa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa 
katika wilaya ya Hai.  
 Baadhi
 ya wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia 
fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wakinyanyua mikono 
kuashiria kuunga mkono kampeni hiyo.  
 Diwani
 wa kata ya Masama Kusini Elingaya Masawe (Chadema) akizungumza wakati 
wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika 
shule za msingi na sekondari wilayani Hai.  
 Diwani
 wa kata ya Bomang'ombe ,Joe Nkya (Chadema) akizungumza wakati wa 
uzinduzi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 
vya madarasa uliofanyika katika shule ya msingi Msamadi wilayani Hai. 
 Makamu
 mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Diwani wa kata ya Machame
 Magharibi Goodluck Kimaro (Chadema) akizungumza katika uzinduzi huo.  
 Mkuu
 wa wilaya akizungumza namna wanavyoshirikiana na Madiwani wa upinzani 
katika shughuli za menedeleoo ya wananchi wilayani Hai.kulia kwake ni 
Diwani wa kata ya Masama Mashariki ,John Munis (Chadema). 
 Mkuu
 wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akitoa maelezo juu ya namna wananchi
 watakavyo changia katika ujenzi wa madarasa kwa njia ya harambee ili 
kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.  
 Baadhi
 ya wananchhi waliofika katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi 
wa vyumba vya madarasa wakitoa ahadi zao wakati wa harambee ya 
kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo.  
 Mkuu
 wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongoza harambee ya kuchangia 
ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Msamadi iliyopo katika kijiji 
cha kwa sadala.  
 Baadhi
 ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakifuatilia matukio mbalimbali 
yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba 
vya madarasa.  
 Ujenzi wa vyumba vya madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msamadi iliyopo kijiji cha Kwa Sadala wilayani Hai.  
 Mafundi
 ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro 
Said Mecky Sadiki pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.  
 Baadhi
 ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakiwa katika picha ya pamoja na
 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya
 ya Hai ,Gelasius Byakanwa mara baada ya kumalizika kwa harambee ya 
kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo Swissport wametoa kiasi 
cha Sh Mil 15. 
 
 
 
 
 
  
 
 
 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni