Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun akipewa maelezo na Afisa
Mipaka Holili Michel Amo, juu ya jiwe linaloonyesha mpaka wa Tanzania
na Kenya lililopo katika mpaka wa Holili ambalo limekua likisogezwa na
watu wasiojulikana hivyo kuharibu alama za mipaka. Naibu waziri Masauni
amesema kuwa licha ya changamoto zinazojitokeza katika mipaka yote
miwili ni lazima kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye mipaka hiyo na
kudhibiti njia zote zisizo rasmi zinazotumiwa na wahamiaji haramu pamoja
na wafanyabiashara za magendo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni avitaka vyombo vya
ulinzi na usalama nchini kuzidi kuimarisha ulinzi katika mipaka ili
kushirikiana na Serikali katika mpango wa kupambana na uhalifu nchini.
Masauni aliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara katika mipaka ya Tarakea na Holili iliyopo mkoani Kilimanjaro ili kujione changamoto zinazojitokeza katika mipaka hiyo ambapo tarifa zinaonyesha kwamba kuna njia zisizo rasmi zaidi ya 265 zinazotumiwa kuptisha bidhaa za magendo na wahamiaji haramu
Katika ziara hiyo Naibu Waziri Masauni alivitaka vyombo vyote vya ulinzi na Usalama nchini kuhakikisha vinaashirikiana kila mtu kwa nafasi yake ili kupambana na uhalifu wa kupitisha bidhaa za magendo zinazopitishwa katika mipaka hiyo na kuikosehsa serikali mapato.
Masauni alisema kuwa Serikali ya awamu ya Tano ina dhamira ya kupeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo ni lazima kwa vyombo hivyo kudhibiti biashara zote zinazopita kimagendo mipakani humo lakini pia kuepuka rushwa ili kupiga hatua mbele za kimaendeleo.
Pamoja na kuwapo kwa changamoto ya nguvu kazi na vitendea kazi serikali itahakikisha inaaandaa maofisa wa kutosha mipakani humo ili kuongeza nguvu kazi wakati wa operesheni zao na doria wakati wote.
Aidha Masauni ametoa rai kwa watumishi wa vyombo hivyo kujiepusha na tabia ya kushirikiana au kuwaficha wafanyabiaashara wanao jihusishaa na biashara ya maagendo.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimaanjaro Kamishna Msaidizi Mwqaandanizi Wilbrod Muutafungwa almueleza naibu Waziri huyo licha ya changamoto zilizopo wanaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipaka kwa kufanya doria mara kwa mara licha ya kwamba wafanyabiashara hao wa bidhaa za magendo kutumia mbinu mbalimbali kukwepa ushuru lakini Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limeweza kuwatia mbaroni.
MASAUNI ALITAKA JESHI LA MAGEREZA KUTEKA SOKO NDANI YA NCHI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaun aagiza Jeshi la Magereza kuzidi kuboresha viatu vinavyotengenezwa na kiwanda chao ili kujipatia soko kubwa ndani ya nchi na nje.
Hayo aliyasema jana kwa wakuu wa Gereza la karanga na viongozi wa kiwanda hicho alipofanya ziara yake ya siku moja katika kiwanda cha viatu kilichopo katika gereza hilo, mkoani Kilimanjaro
Aidha, Naibu Waziri huyo alisisistiza Jeshi hilo kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kuhakikisha majeshi yote nchini yanatumia viatu vinavyozalishwa na Jeshi la Magereza, hivyo ni muhimu kuendelea kuzalisha bidhaa zilizo bora zaidi
Haiingii akilini maofisa wa majeshi mbalimbali nchini kuagiza viatu nje ya nchi wakati viwanda vya ndani vinauwezo wa kuzalisha viatu bora zaidi vinavyodumu kwa muda mrefu kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi, alisema Masauni.
Masauni alisema kwamba dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati hivyo Jeshi la Magerezaa kupitia kiwanda chake na miradi mingine mingi halina budi kuendelea kuzidisha kuzalisha viatu bora vitakavyo kidhi kiwango cha uhitaji na soko ili kukuza uchumi wao na Serikali kwa ujumla.
Aidha, katika ziara yake, Naibu Waziri Masauni amesisitiza kuwa ni muhimu Jeshi hilo kufanya miradi mingi kwa ustadi mkubwa ili kujipatia psa zitakazosaidia kujiendesha wao kama jeshi na mashirika mengine yanayounga mkono miradi yao hivyo kutotegemea ruzuku kutoka serikalini.
Waziri huyo alilipongeza Jeshi hilo kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora kulinganisha na nyingine zinazoingizwa nchi, hivyo amesisitiza kuzidi kutengeneza viatu bora zaidi ili kuwa na uwanja mpana wa soko la ndani nan je ya nchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni