Waziri
 wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine 
Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Katibu 
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe.Said Djinnit. 
Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa 
Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Oktoba, 2016.
Mkurugenzi
 Msaidizi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na 
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Omary Mjenga (wa kwanza kushoto), 
Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya 
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ally Ubwa kwa pamoja 
wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Bw. Djinnit 
(hawapo pichani).
 
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Bw.Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni