Mradi wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu. Kwa Mkoa wa Arusha, mradi huu utawanufaisha wafugaji wa Wilaya tatu za Monduli, Longido na Ngorongoro.
Lengo la Mradi wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ni kuziwezesha Wilaya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hususani jamii za kifugaji.
Mradi utawezesha maeneo kame (dry lands) kupata njia mbadala ya ustahimilivu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi katika kuchangia usalama wa chakula na uchumi imara wa wananchi.
Vilevile kuwezesha wana jamii ya kifugaji kupanga mipango yenye kuzingatia matumizi bora ya Rasilimali walizonazo.
Mambo muhimu yanayozingatiwa katika mipango hiyo ni pamoja na upatikanaji wa maeneo ya malisho na upatikanaji wa maji unaozingatia utawala wa maeneo na usuluhishi wa migogoro juu ya matumizi ya Rasilimali.
Mradi huu utawezesha halmashauri hizi tatu kuandaa mipango ya miradi ya maendeleo itakayoweza kukabiliana na athari za tabia nchi katika jamii hizi za wafugaji.
Shirika la Hakikazi Catalyst na Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) yatashirikiana na halmashauri hizi tatu kuwezesha mradi huu kwa halmashauri tatu za Mkoa wa Arusha kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2016 hadi 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni