Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
 (kulia)akipokea mmoja wa Miongoni mwa Misahafu elfu kumi iliyotolewa na
 Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,mara baada ya Swala ya Ijumaa 
iliyoswaliwa leo katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme 
Mohammed VI akiwa katika ziara ya kibinafsi na ujumbe wake, ambapo 
amefikia katika Park Hyatt Hotel- Shangani Mjimkongwe wa Zanzibar,[Picha
 na Ikulu.]28/10/2016.
Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
 na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, (katikati) pamoja na Viongozi mbali 
mbali na Ujumbe wa Mfalme wakijumuika na Waislamu wengine wakiswali 
swala ya Ijumaa iliyoswalishwa na Sheikh Fadhil Soraga katika  Msikiti 
wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo Nchini kwa  ziara 
ya kibinafsi
Mfalme wa
 Morocco, Mohammed VI(kulia) akisalimiana na  Katibu wa Mufti wa 
Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga mara baada ya kuswalisha Swala ya Ijumaa 
katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja,Mfalme Mohammed VI yupo 
Nchini kwa  ziara ya kibinafsi
Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
 (kushoto) akifuatana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, pamoja na Mkuu 
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (kulia) wakitoka 
nje ya Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja baada ya swala ya Ijumaa leo
Rais wa 
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
 (kushoto) akiagana na Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, mara baada ya 
kumalizika kwa swala ya Ijumaa leo katika  Msikiti wa Mwembeshauri Mjini
 Unguja,Mfalme wa Morocco, Mohammed VI yupo nchini na ujumbe wake kwa 
ziara ya kibinafsi Zanzibar.
Baadhi ya
 Viongozi wa Serikali walihudhuria katika swala ya Ijumaa katika Msikiti
 wa Mwembeshauri Mjini Unguja leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed 
VI,na ujumbe wake waliswali kwa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
 wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Baadhi ya
 Viongozi wa Dini wakiwa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Unguja 
leo,ambapo Mfalme wa Morocco, Mohammed VI,na ujumbe wake waliswali kwa 
pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj 
Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 28/10/2016.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni