Rais Dkt John Pombe Magufuli ameandika historia kwa wananchi tangu Tanzania ipate uhuru na tangu atimize mwaka 1 madarakani kwa kuipatia Wilaya ya Ngorongoro barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 60 tangu Wilaya hiyo ianzishwe.
Haya yameelezwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha 38 cha bodi ya barabara cha Mkoa huo.
Gambo alisema barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami na itaunganisha mji wa Wasso hadi Sale kilomita 60 imepata Baraka zote kutoka kwa Rais Magufuli.
Gambo ameeleza katika Kikao hicho kwamba Rais Magufuli ameagiza kuanza kujengwa kwa barabara hiyo mara moja kwa kiwango cha lami kama alivyoahidi wakati wa Kampeni alipokuwa katika Wilaya hiyo.
Amesema barabara hiyo inatarajiwa kutekelezwa na Wakala wa barabara mkoani Arusha ( TANROADS).
Mkuu huyo wa Mkoa amesema hii ni hatua muhimu sana kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro ,Wilaya haina hata barabara moja yenye kiwango cha lami.
Mkuu huyo wa Mkoa pia alisema fedha zinazotolewa na wafadhili benki ya dunia sio msaada bali ni fedha za mkopo kwa Tanzania ambazo Tanzania italazimika kuzilipa hapo baadaye.
Akitoa shukrani zake mbunge wa jimbo la Ngorongoro Tate William Ole Nasha alisema kwa mala ya kwanza Ngorongoro inapata barabara yenye kiwango cha lami, kweli itakuwa furaha kubwa sana kwa wananchi wa Wilaya hito.
Wilaya ya Ngorongoro ni kati ya Wilaya sita za Mkoa wa Arusha ambapo Wilaya hii inakabiliwa na matatizo makubwa ya miundo mbinu ya ukosefu wa barabara za uhakika ambapo usafiri katika Wilaya hiyo ni wa kubahatisha kutokana na kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika ya barabara kwenda maeneo ya vijijini.
Hivi sasa TANROADS inahudumia kiasi cha kilomita 1,220 katika Wilaya za Mkoa wa Arusha zikiwemo barabara kuu na barabara za Mkoa alisema Meneja wa Mkoa Mhandisi John Kalupale.
Wajumbe wa bodi ya barabara ya Mkoa wa Arusha wakisikiliza agenda mbalimbali zikijadiliwa za kikao cha 38 cha bodi hiyo. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni