MAHAKAMA
Kuu Tanzania, Divisheni ya Ardhi, imetupilia mbali maombi ya Kampuni ya
Mbowe Hotels Limited inayomikiwa na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka kurudishwa
kwenye jengo la Billicanas kwa sababu waliondolewa katika jengo la
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kufuata taratibu zote za kisheria.
Aidha,
Jaji Sivangilwa Mwangesi alisema shirika hilo lilifuata taratibu zote
kumwondoa mlalamikaji katika jengo hilo na kwamba inashikilia mali zake
kihalali hadi atakapolipa kodi ya Sh.Bilioni 1.3 kama anavyodaiwa.
Akisoma
uamuzi huo mapema jana Jaji Mwangesi baada ya kusikiliza hoja za pande
zote mbili, mahakama yake iliamua kutupilia mbali maombi hayo
yaliyofunguliwa chini ya hati ya dharula bila kulipwa gharama.
Jaji
alisema madai ya mlalamikaji kwamba aliondolewa kinyume cha sheria
katika jengo hilo na kampuni ya udalali isiyosajiliwa hayana mashiko
kisheria mahakama inafutilia mbali kesi hiyo.
“Mahakama
hii baada ya kupitia hoja za pande zote mbili imeona kwamba mlalamikiwa
wa kwanza NHC alifuata taratibu zote kumtoa mlalamikaji katika jengo
hilo … pia imeona kwamba kampuni ya udalali Foster Auctioneers and
General Traders ilifanyakazi ya kuondoa mali zake kihali, inatupilia
maombi haya bila kulipwa gharama ya kesi hii” alisema Jaji Mwangesi.
Aidha
akifafanua zaidi jaji alisema pamoja na madai ya kuwepo kwa mkataba
kati ya NHC na Mbowe, mkataba huo haukuwahi kutekelezwa kwa hiyo ni sawa
na kwamba haupo.Upande wa mlalamikaji uliongozwa na Mawakili Peter Kibatala akisaidiana na John Mallya.
Upande wa walalamikaji uliongozwa na Mawakili Aloyce Sekule, Aliko Mwamanenge na Mariam Mungura.Wakili
Mwamanenge akizungumza na Blogu ya Jamii nje ya viunga vya mahakama
hiyo, alisema mlalamikaji alisema mahakama imetenda haki na kwamba
mlalamikaji alidai kuwa na mkataba kati yake na NHC, lakini mahakama
hiyo imeona mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.
“Mahakama
imeona dalali alifanya kazi yake kwa kufuata taratibu za kisheria na
hata hizo mali zinashikiliwa na mteja kihalali hadi atakapolipa deni la
Sh. Bilini 1.3 ndipo atarejeshewa mali hizo” alisema wakili Mwamanenge.
Kwa
upande wake Wakili Mallya alisema wamewasilisha maombi ya kuomba nakala
ya uamuzi ili waombe marejeo Mahakama ya Rufani Tanzania.
Pia,
wamepeleka maombi ya kuomba chochote kisifanyike katika jengo hilo na
kuhusu mali za Mbowe ni mpaka uamuzi utakapotolewa na Mahakama ya Rufani
dhidi ya maombi yao ya marejeo.
Alisema
Jaji katika uamuzi wake amesema mkataba kati ya NHC na Mbowe haukuwahi
kutekelezwa na haupo kisheria kwa hiyo tunasubiri nakala ya uamuzi
tuupitie ili tuwasilishe maombi ya marejeo mahakama ya juu” alisema
Wakili Mallya.
Maombi
hayo yaliyosajiliwa mahakamani hapo kwa namba 722 ya 2016 dhidi ya NHC,
yalifunguliwa chini ya hati ya dharula baada ya Mbowe kuondolewa kwenye
jengo hilo mapema Septemba Mosi, mwaka huu.
Katika
hati ya kiapo Mbowe alidai kwamba yeye na mlalamikaji katika mgogoro
huo warejee kwenye usuluhishi kwa mujibu wa mkataba wa ubia huo.
Hata
hivyo, upande wa walalamikiwa ulipinga hatua hiyo kutokana na
kutokuwepo kwa nyaraka hizo mahakamani hapo juu ya mwenendo wa mchakato
huo wa usuluhishi, kwani walitoa ilani ya kumuhamisha Mbowe katika jengo
hilo kwa kufuata sheria.
Pia
ilidaiwa kuwa Mbowe katika jengo hilo ni mpangaji na hata mkataba wa
ushirikiano unaodaiwa umefanyika kati yao kwa sasa hauwezi kufanyakazi
kwa kuwa ulishakwisha muda wake.Katika
madai ya msingi Mbowe alidai kuwa si mpangaji katika jengo hilo, bali
ni mmbia ambaye anamiliki asilimia 75 katika uendeshaji wake huku NHC
wakimiliki asilimia 25.
Hoja
nyingine alidai kuwa, hata kama angekuwa anadaiwa kodi kama wanavyodai
NHC, kuondolewa kwake kulifanywa bila kuzingatia sheria kwani hakukuwa
na amri ya mahakama inayowapa walalamikiwa nguvu ya kisheria ya
kumwondoa.
Kwa
upande mwingine, Mbowe kupitia hati ya kiapo alisema hadaiwi hata senti
tano na NHC kama pango la jengo la Billcanas, na kwamba amekuwa akilipa
tozo zote zinazotakiwa kwa mujibu wa mkataba baina yake na shirika
hilo.
Kwa
mujibu wa hati ya kiapo aliyoiwasilisha mahakamani, mmiliki huyo wa
Kampuni ya Mbowe Hotels Ltd alidai kwa mujibu wa mkataba wa ubia wa
pande hizo mbili, anapaswa kuwalipa NHC mapato ya jengo kila mwezi.
Katika
hati hiyo, Mbowe alisema hadaiwi fedha yoyote kwani amekuwa akitekeleza
matakwa hayo ya kimkataba kama yalivyosainiwa mwaka 1997, huku
akiambatanisha ushahidi wa risiti ya fedha ambazo amekuwa akilipa.
UPDATES...
Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii
Globu ya Jamii
Mahakama
Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe
Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa Shirika hilo
liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa
kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.
Uamuzi
huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema
madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba
mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.
Jengo tajwa lilikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania daima na klabu ya Usiku ya Billicanas. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Mhe. Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.
Jengo tajwa lilikuwa na ofisi za gazeti la Tanzania daima na klabu ya Usiku ya Billicanas. Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Mhe. Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.
Amesema
katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana
na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa
Mbowe Hotels.
Mlalamikaji
alikuwa wakidai kwamba wakati NHC inamtoa kwenye nyumba alikuwa ndani
ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa
Mkataba wa Ubia Ulikuwepo kwa kuwa haukutekelezwa ipasavyo.
Na kwamba wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya Utekelezaji wake.
Na kwamba wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya Utekelezaji wake.
Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC. Amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.
Nae Wakili upande wa Mbowe Hotels, John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi. Amesema kuwa nakala wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa mapema iwezekanavyo.
Wakili
wa NHC, Aliko Mwamnenge akizungumza na waandishi habari baada ya kutoka
katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikihusu maombi ya Mbowe hotels kurejea
katika ofisi zake,ambapo hukumu yake imetolewa leo katika mahakama kuu
kitengo cha Ardhi,jijini Dar.
Wakili
wa Mbowe Hotels, John Malya akizungumza na
waandishi wa habari juu ya hukumu iliyotelewa na Mahakama kuhusiana na
maombi ya kurejea Mbowe hotels na Mali zake, katika mahakama kuu
kitengo cha ardhi leo jijini Dar es salaam.
Mawakili wakitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa.
Mawakili wa Mbowe Hotels John Mallya (kushoto) na Peter Kibatala (kulia) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni