Askari waliokuwa mafunzoni 59 pamoja
na walinzi wameuwawa na wapiganaji walioshambulia chuo cha polisi
nchini Pakistani katika mji wa Quetta.
Wapiganaji watatu waliokuwa
wamevalia fulana zenye mabomu, waliingia kwenye chuo hicho na
kutekeleza shambulizi hilo.
Operesheni kubwa ya kijeshi
ilifanyika kwa saa kadhaa ambapo wapiganaji hao nao wameuwawa, huku
watu wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa.
Mmoja wa majeruhi akibebwa na askari wenzake nchini Pakistani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni