Hatimaye
mazishi ya kuuaga mwili wa Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Dk.
Didas Masaburi, yamewakutanisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kwa kusalimiana na
kushikana mikono.
Tukio
hilo la aina yake liliwafanya watu mbalimbali waliokuwa katika msiba
huo kubaki wakishangaa, hasa baada ya Rais mstaafu Kikwete kumfuata
Lowassa na kumwuliza hali rafiki yake huyo wa zamani waliokulia wote
CCM.
Tangu
wakati huo viongozi hao ambao walikuwa marafiki wa karibu tangu ujana
wao walikuwa wakirushiana vijembe ambapo jana walikutana ana kwa ana
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa kuuaga mwili
wa Dk. Masaburi kabla ya kwenda kuzikwa nyumbani kwake Chanika Manispaa
ya Ilala.
Akiwa
katika viwanja hivyo, Kikwete alipomwona Lowassa akiingia viwanjani
hapo alinyanyuka na kumfuta Lowassa katika kiti chake kisha kusalimiana
naye kwa kupeana mikoni huku wakizungumza.
Lowassa
aliyekuwa ameketi jirani na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
pamoja na mkewe Regina Lowassa, alisimama na kumjibu salamu.
Kwa
muda mrefu wanasiasa hao ambao wamewahi kuwa marafiki hadi kupewa jina
la utani ‘Boys II Men’, waliingia katika uhasama kwa kile kinachodaiwa
ni kusalitiana kisiasa.
Urafiki
wa wawili hao ulianza kuingia doa mwaka 2008 wakati wa kashfa ya
Richmond iliyosababisha Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu kwa kile
alichoeleza ni kunyimwa haki ya kusikilizwa baada ya kuibuka kwa kashfa
hiyo kwa kile alichodai ilikuwa ni vita ya kutaka ‘uwaziri mkuu’.
Ukaribu
wa Lowassa na Kikwete uliendelea kupungua na kuwa shakani zaidi wakati
wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana baada ya Lowassa kukatwa jina lake katika
kinyang’ anyiro cha kuwania nafasi ya kugombea urais kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na kuamua kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Kwa
takribani mwaka mmoja sasa tangu mchakato wa ndani wa CCM wa kumpata
mgombea wake wa urais Julai 10, mwaka jana umalizike wawili hao
hawajawahi kukutana hadharani na kupeana mikono.
Katika
mchakato huo Kamati Kuu ya CCM iliyokutana hadi usiku wa manane
iliibuka na jibu kwamba, jina la Edward Lowassa limekatwa katika watu
wanaowania urais kupitia chama hicho.
Waliopitishwa
na kuingia tano bora na Kamati Kuu walikuwa ni Bernard Membe, Dk John
Magufuli, Dk Asha Rose Migiro, January Makamba na Amina Salum Ali, huku
makada wengine 33 wakitupwa akiwamo Lowassa.
Kutokana
na hali hiyo Lowassa alichukua aumuzi mzito wa kuihama CCM, Julai 28,
mwaka jana na kujiunga na Chadema na hatimaye kuteuliwa kuwa mgombea
urais kupitia chama hicho cha upinzani akiungwa mkoano na vyama vinaunda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni