Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa nne kutoka kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Mawaziri wenzake wa Fedha kutoka nchi 54 za
Kiafrika, wanaohudhuria Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya
Korea na nchi za Afrika (KOAFEC), unaofanyika Jijini Seoul, Korea
Kusini.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika anayeiwakilisha Tanzania (AfDB)
Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) wakimsikiliza kwa makini Raisi wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kabla ya kuanza kwa mkutano
unaojadili namna kilimo na mapinduzi ya viwanda vinavyoweza kuibadili
Afrika Kiuchumi na Kijamii wakati wa Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa
Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika (KOAFEC) unaofanyika Jijini
Seoul, Korea Kusini.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akitia saini
makubaliano ya uteuzi wa mradi utakao fadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki
ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Korea, wenye thamani ya
dola Milioni 50 za Marekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18
zitakazotumika kujenga njia ya usafirishaji umeme kwanjia ya gridi ya
Taifa, yenye msongo wa kV 400 katika ukanda wa kaskazini Magharibi
itakayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Mkoani Kigoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa na
Mawaziri wenzake kutoka nchi za Kenya, Uganda na Ethiopia (wengine
hawako Pichani) wakionesha kwa waandishi wa habari (hawako pichani pia)
nyaraka za makubaliano ya uteuzi wa mradi utakao fadhiliwa kwa pamoja
kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Korea, wenye
thamani ya dola Milioni 50 za Marekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni
100.18 zitakazotumika kujenga njia ya usafirishaji umeme kwa njia ya
gridi ya Taifa, yenye msongo wa kV 400 katika ukanda wa kaskazini
Magharibi kwa upande wa Tanzania itakayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi
hadi Mkoani Kigoma. wakati wa Mkutano wa 5 wa ushirikiano wa Kiuchumi
kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika, unaoendelea Jijini Seoul Korea
Kusini.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na
Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee
Duk-Hoon, wakitia saini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola
za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za
Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji
taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi
kati ya Korea na nchi za Afrika, unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na
Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee
Duk-Hoon, wakipeana mikono baada ya kusaini Mkataba wa mkopo wenye
masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya
shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa
Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa
Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika,
unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na
Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee
Duk-Hoon, wakionesha mkataba waliousaini wa mkopo wenye masharti nafuu
wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194
za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa
maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa
Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika, unaoendelea Jijini Seoul,
Korea Kusini
Baadhi
ya wajumbe kutoka Tanzania na Korea walioshuhudia utiawaji saini wa
mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092
sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi
wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam,
wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za
Afrika (KOAFEC), unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini.
Benny Mwaipaja, WFM, Seoul, Korea
TANZANIA,
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Korea ya Kusini zimetiliana
saini makubaliano ya pamoja kutekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya umeme
gridi ya Kaskazini Magharibi inayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi
Kigoma, yenye msongo wa kV 400 mbapo Serikali ya Korea imeahidi kutoa
Dola zaMarekani milioni 50 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18, kwa
ajili ya kugharamia mradi huo.
Hali kadhalika, Tanzania na
Benki ya Exim ya Korea, zimesaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu
wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni
194 za Tanzania, kwaajili ya mradi wa Upanuzi waMiundombinu ya mfumo wa
maji taka Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wa Tanzania,
Makubaliano pamoja na Mkataba vimesainiwa na Mhe. Dkt. Philip Mpango
(MB) Waziri wa Fedha na Mipango kwa niaba ya Serikali, Oktoba 25, 2016
Jijini Seoul nchini Korea Kusini huku upande wa AfDB, aliye saini ni
Rais wa Benki hiyo Adesina Akinwumi, na kwa upande wa Benki ya Exim,
mkataba huo umesainiwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki hiyo
Lee Duk-Hoon.
Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano
na mkataba huo, Dkt. Mpango amesema makubaliano na mkataba
vilivyosainiwa vina manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.
“Wananchi
wa Upande ule waanze kufurahia kwamba maendeleo yanakuja na hasa
tunaposema maendeleo ya viwanda ambavyo nilazima vitumie umeme, na
kwamba mradi huu unatarajia kupelekwa hadi Mbeya” Amesisitiza Dkt.
Mpango.
Dkt. Mpango, amesema kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa
pia kwakuwa serikali imedhamiria kuufungua ukanda wa Magharibi mwa
Tanzania, kwa upande wa viwanda vya aina mbalimbali.
Kwa upande
wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uwekezaji) wa Shirika la Ugavi wa Umeme
nchini Tanzania-TANESCO, Decklan Mhaiki, amesema mradi wa umeme wa
Nyakanazi hadi Kigoma utakuwa na urefu wa kilometa 280 na utakapo
kamilika utaondoa changamoto ya shirika hilo kuzalisha umeme unatumika
katika ukanda huo wa Magharibi hususan Kigoma, kwa kutumia majenereta
ambayo uendeshaji wake ni ghali na umeme wake si wa uhakika.
“Kuleta
laini kama hii, kwanza itapunguza gharama kubwa, na umeme wa ziada
utakao zalishwa tunaweza kuuza nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia
Congo, upande wa pili wa Ziwa Tanganyika, lakini kikubwa ni
kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika”
ameongeza Bw. Mhaiki.
Akizungumzia mkataba wa ujenzi wa
miundombinu ya maji taka Jijini Dar es salaam, Dkt. Philip Mpango,
amebainisha kuwa mradi huo unatarajia kuwa na tija kwakuwa utatatua
changamoto ya majitaka kutuama mitaani hasa wakati wa mvua na
kusababisha magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu.
Akifafanua
kuhusu mradi huo, Mchumi ambaye pia ni Afisa anayeshughulika na
utafutaji wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Melckzedek
Mbise, amesema kuwa mradi wa maji wa Ruvu unatarajia kuongeza wingi wa
maji Jijini Dar es salaam, utakaosababisha uzalishaji wa maji taka pia
kuongezeka, hivyo mradi huo wa kuondoa maji taka umekuja wakati muafaka.
“Mradi huu umekuja wakati muhimu na mkopo una masharti nafuu sana” Amesisitiza Bw. Mbise.
Naye
Afisa Mkuu wa utafutaji rasilimali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango
Zanzibar, Sabra Issa Machano, amesema kuwa kati ya nchi 54 za Kiafrika
zinazohudhuria mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea
naAfrika, Mjini Seoul Korea, ni nchi nne tu zilizopewa mkopo na ufadhili
ambazo ni Kenya, Uganda na Ethiopia, huku Tanzania ikipewa kiasi
kikubwa zaidi cha fedha jambo linaloonesha kuwa Tanzania inakubalika
Kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni