Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala
 akiwa anazungumza na waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la 
Saratani ya shingo ya Kizazi, katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini 
Arusha.,aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mountmeru iliyopo jijini Arusha.
 Waandishi
 wa habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa 
Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala,Aliyepo 
kushoto kwake ni Dkt.Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital
Waandishi
 wa habari wanawake wakifuatilia kwa karibu baadhi ya majibu ya 
yaliyokuwa yakijibiwa na madaktari walioendesha mafunzo,mafunzo hayo 
yalikwenda sambaba na upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi.
Na Mahmoud Ahmad Arusha.
  
Na Mahmoud Ahmad Arusha.
Naibu
waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la
ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV
vinavyosababisha   Saratani ya mlango wa
kizazi
Kigwangala
amesema
 wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango
 wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila 
kinga,huambukizwa  kwa kujaamiana .
Kigwangala amesema  kuwa
 kati ya wanawake 100,000 wanawake 50.9% wanaweza kupata saratani ya 
Shingo ya kizazi,na kati ya hao asilimia 37.5% wanapoteza maisha hivyo serikali imeanza kutekeleza utafiti
wa mradi ambao utahusisha wasichana wenye umri kati ya miaka 9-14 katika wilaya
ya Moshi na utakapokamilika wataanza utoaji wa chanjo hiyo kwa nchi nzima,amewataka
kutokufanya ngono mapema.
Amesema
kuwa Saratani ya mlango wa kizazi haionyeshi dalili wala maumivu yeyote amesema
mgonjwa anaweza akawa nao kuanzia miaka 10-15 bila kujitambua huku dalili
zikiwa zinakwenda taratibu sana.
Kwa upande
wake Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya mount Meru amesema kuwa dalili za
Sratani ya Mlango kizazi ni kutokwa na damu bila mpangilio,kutokwa na majimaji
yenye harufu kali,amewataka wanawake watakapoziona dalili hizo wawahi hospitali
mapema kabla tatizo halijawa kubwa.
Aidha
Masumuni amesema kuwa unaweza kujikinga ili usipate saratani ya mlango wa
kizazi kwa kupima saratani ya mlango wa kizazi mapema,kupunguza idadi ya kuzaa
watoto wengi,kupunguza idadi ya wpenzi wengi,ukifanya ngono watumie kinga.
Sambamba
na hayo Dkt.Mwanahamisi Lyinga amesema kuwa zipo njia kuu tatu za kupima
saratani ya mlango wa kizazi mabazo ni pamoja na kutumia Darubini,Upimaji wa(
DNA)wa kirusi,pamoja na Via utambuzi wa kuona kwa kutumia Siki.
Kwa upande
wake Sr.Noela Lyinga ambaye ni muuguzi katika hospitali ya Mountmeru ametoa
elimu kwa wanawake wawe wanajikagua matiti yao kila wanapomaliza mzunguko wao
wa hedhi kila mara ili kuona kama yapo mabadiliko katika matiti yao ambayo yanaweza
kuleta saratani ya matiti.
Lyinga
amewataka wanawake mara wanapoona dalili yeyote 
ambayo siyo ya kawaida katika matiti yao wasisite wawahi hospitali
mapema wakafanyiwe uchunguzi na vipimo ili kama utagundulika ugonjwa waweze
kupatiwa matibabu kwa haraka zaidi. .



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni