Na Dotto Mwaibale
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imechukua usimamizi wa Benki ya Twiga 9Twiga Bancop Limited) kuanzia Oktoba 2016 imefahamika.
Hayo
 yamebainishwa na Gavana wa Tanzania, Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam 
leo jioni wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari 
kuhusu hatua hiyo ya kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo serikali ilikuwa 
ikiimiliki kwa asilimia 100.
"Kwa
 mamlaka iliyopewa benki kuu chini ya kifungu cha Sheria namba 56 (1) 
(g) (i) na 56 (2) (a)-(d) cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya 
mwaka 2006 benki kuu ya Tanzania imeamua kuchukua usimamizi wa benki 
hiyo kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016" alisema Ndulu.
Alisema
 uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki hiyo ina upungufu 
mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za 
Fedha ya mwaka 20016 na kanuni zake.
Alisema
 upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia 
kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hiyo kutahatarisha usalama 
wa amana za wateja wake.Profesa Ndulu alisema kutokana na uamuzio huo 
Benki Kuu ya Tanzania imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa 
benki hiyo na imemteua Meneja Msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la 
kusimamia shughuli za benki ya Twiga kwa kipindi ambacho itakuwa chini 
ya usimamizi wa benki kuu.
Alisema
 pia Umma unaarifiwa kuwa katika kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki 
moja kuanzia siku ya taarifa hii, shughuli za utoaji wa huduma za 
kibenki za benki hiyo zitasimama ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga 
taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.
Alisema
 Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea 
kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta 
ustahimilivu katika sekta ya fedha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni