Ugomvi baina ya mashabiki wa West
Ham na Chelsea umeibuka mwishoni mwa mchezo wao wa jana wa kombe la
EFL, ambao Chelsea walilala kwa magoli 2-1 kwenye dimba la London.
Chupa za plastiki na viti vilirushwa
na mashabiki mwishoni mwa mechi hiyo huku mamia ya mashabiki wakorofi
wakihusika na tukio hilo baya kutokea katika soka.
Katika mchezo huo Cheikhou Kouyate
alifunga kwa kichwa kabla ya mapumziko na kisha Edimilson Fernandes
akaongeza la pili kwa shuti la yadi 18 huku Gary Cahill akiifungia
Chelsea goli pekee katika dakika ya 90.
Kipa wa Chelsea akiruka bila ya mafanikio kuzuia mpira wa kichwa uliopigwa na Cheikhou Kouyate
Edimilson Fernandes akiachia shuti lililzaa goli la pili la West Ham
Mashabiki wakizozana punde tu baada ya kumalizika kwa mechi hiyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni